Hamad Rashid aiwekea CUF pingamizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid aiwekea CUF pingamizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 23, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed


  Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed na wenzake 10, wamewasilisha Mahakama Kuu mapingamizi ya kisheria, wakidai kiapo kilichowasilishwa na Wakili Twaha Taslima anayewawakilisha wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) katika kesi dhidi ya wadhamini hao, kina upungufu wa kisheria.

  Kiapo hicho cha Taslima kinajibu hoja ya Hamad na wenzake kuhusu maombi madogo katika kesi ya msingi waliyoyawasilisha mahakamani hapo dhidi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF, akiwamo Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

  Hati ya mapingamizi hayo iliyowasilishwa mahakamani hapo na wakili anayemwakilisha Hamad na wenzake katika kesi hiyo, Augustino Kusalika, imedai upungufu mmojawapo uliomo kwenye kiapo hicho cha Taslima, ni pamoja na kuweka masuala ya kisheria kwenye kiapo.

  Upungufu wa mwingine, hati hiyo inadai kuwa ni Taslima kutokutaja chanzo cha habari kilichomueleza mambo aliyoyaeleza kwenye kiapo hicho.
  Hamad na wenzake, wanaiomba mahakama iwaamuru wajumbe hao wa Baraza Kuu kufika mahakamani kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua, ikiwamo kufungwa jela kwa kukiuka amri halali ya mahakama.

  Amri hiyo ya mahakama ilizuia kufanyika kwa mkutano wa Baraza Kuu, Januari 4, mwaka huu, Zanzibar, hadi hapo kesi ya msingi iliyofunguliwa na Hamad na wenzake itakapoamuliwa na mahakama. Hata hivyo, mkutano huo ulifanyika ambapo pamoja na mambo mengine, uliwavua uanachama Hamad na wenzake.

  Katika kiapo chake, Taslima pamoja na mambo mengine, anamtaka Hamad na wenzake kuthibitisha amri hiyo ya mahakama inayodaiwa kuwa ilipelekwa katika ofisi za CUF, Buguruni, jijini Dar es Salaam, Januari 4, mwaka huu na kukataliwa kupokelewa, kama kweli iliwafikia wajumbe hao wa

  Baraza Kuu kwa wakati, kama walivyodai katika hati yao ya maombi.
  Wakati huo huo, kesi ya mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila na wenzake, imeahirishwa hadi Machi 15, mwaka huu.
  Kesi hiyo inayowakabili wadhamini wa Chama cha NCCR-Mageuzi, iliahirishwa jana na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, kutokana na jaji anayeisikiliza, Alice Chinguile, kuwapo safarini.

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  R.i.p. Cuf
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Kwishney!!
   
 4. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Raia wema wa iliyokuwa CUF wafanye fasta wajiunge na chama cha ukombozi dhidi ya magamba, chama kitakachodumisha demokrasia na kuleta maendeleo kwa wananchi wote!
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Umekusudia nini mkuu ( R.i.p. Cuf) Hajafa bado Mzee Hamad Rashid Mbunge wa Wawi. Unamuuwa kabla ya siku zake?Mkuu
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Mkuu, biblia (ambayo Ustaadh wangu Mtatiro anaiamini japo sio sana) inasema UFALME UKIJIFITINI UFALME HUO UTAANGUKA. Once again, R.I.P CUF
   
 7. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  na bado tutaona mengi mwaka huu, cuf walidhani kufukuzana ndio dawa na sasa viongozi wakuu wananukia JELA hii yote ni kutokana na selfishness walonayo. Wamekimaliza chama sasa wanatapatapa......Ni vizuri yamewakuta haya kwani walikua wanafanya kazi kwa maazoea....kidogo timua, sasa safari hii wameingia choo cha kike. Wamevamia kisiki cha mpingo hakin'goki....wa pwani wanasema "LIMEWAGANDA'':eyebrows:
   
 8. 1

  19don JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  natamani cuf ifutwe kabisa kwenye daftali la usajili kwa tendwa
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hatutaki waendew CCM ...nani anataka vurugu zao na vipedo vyao vile
   
Loading...