Hamad Rashid aivuruga ADC

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha ADC kimekumbwa na mgogoro mkubwa baada ya wanachama na baadhi ya viongozi wake kuandika barua kwa msajili wa vyama vya siasa nchini na kusema hawamtambui Hamad Rashid kama mlezi wa chama hicho.Barua hiyo kwenda kwa msajili imeelezea ukiukwaji mkubwa wa kanuni uliofanyika.
Baadhi ya viongozi wa ADC walimtangaza Hamad Rashid kama mlezi wa chama hicho katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni.
Chama cha ADC kinatumia bendera inayofanana karibu kwa kila kitu na chama kikuu cha upinzani nchini-CDM chenye idadi kubwa ya wafuasi na inadaiwa chama hicho kilichagua bendera hiyo ili kuwachanganya wananchi na kupata uungwaji mkono kama ule wanaopata wenzao wa CDM

Source:Tanzania Daima
 
Hao walipata baraka zote za CCM ndio maana hata usajili wake ulifanyika haraka haraka na wakapokea usajili kwa mbwembwe nyingi bila hata uhakiki makini wa idadi ya wanachama. Si tunajua nn kilitokea kwa CCJ

acha wavune walichopanda wao walidhani wanaikomoa CDM wakasahau kuwa wanajikomoa na kujiua kisiasa

usishangae jogoo kuwika mjini hiyo ndiyo jadi yake
 
Nazidi kusisitiza habari katika TANZANIA DAIMA' na 'UHURU' zinaegemea upande fulani, ndio maana sizipendi wala kuziamini sana.
 
Hicho chama nilijua tu hakitakuwa na maisha marefu, kimeundwa kwa zengwe! katibu mwenyewe ni kilaza huyo LIMBU
 
Nilisema hapa. Kwa nini kuanzisha chama wakati tayari Chadema inafanya vizuri? Tuendelee kupiga magoti, Mungu atasambaratisha hawa maadui wa nchi yetu kwa vile alivyomshindia Gideoni. Vita hii si yetu.
 
Hivi Hamadi Rashid bado ni mbunge kwa tikiti ya CUF? Inakuwaje awe mlezi wa chama kingine tena?
 
Nilisema hapa. Kwa nini kuanzisha chama wakati tayari Chadema inafanya vizuri? Tuendelee kupiga magoti, Mungu atasambaratisha hawa maadui wa nchi yetu kwa vile alivyomshindia Gideoni. Vita hii si yetu.

CHADEMA kina wenyewe hao wakina 'GIDEONI'! Wengine wanahitaji chama vilevile!
 
Siku zote UKIPANDA UPEPO, BASI UJUE KUWA UTAVUNA DHOLBA.

Pole sana Ba Hamad
 
Chama cha ADC kimekumbwa na mgogoro mkubwa baada ya wanachama na baadhi ya viongozi wake kuandika barua kwa msajili wa vyama vya siasa nchini na kusema hawamtambui Hamad Rashid kama mlezi wa chama hicho.Barua hiyo kwenda kwa msajili imeelezea ukiukwaji mkubwa wa kanuni uliofanyika.
Baadhi ya viongozi wa ADC walimtangaza Hamad Rashid kama mlezi wa chama hicho katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni.
Chama cha ADC kinatumia bendera inayofanana karibu kwa kila kitu na chama kikuu cha upinzani nchini-CDM chenye idadi kubwa ya wafuasi na inadaiwa chama hicho kilichagua bendera hiyo ili kuwachanganya wananchi na kupata uungwaji mkono kama ule wanaopata wenzao wa CDM
Source:Tanzania Daima

Kuna wakati Kingunge Ngombale Mwiru aliwahi kusema hivi, "WAhindi walijiuliza kwanini Wazungu wamendelea/wameendelea? wakapa jibu kua ni kwasababu ya elimu, nao wakajielimisha na sasa wasumbua dunia, Wachina nao wakajiuliza swali hilo hilo, jibu walilolipata linafanana na la wahindi, wakajieleimisha na sasa wanasumbua Dunia, sisi Wafrica tulijiuliza kwanini Wazungu wamenedelea, kabla hatujapata jibu, tukaona tujifunze lugha yao, na sasa tunaendelea kutumia vitu vya" hapo kwenye Bold, hivi CDM inapendwa na watu kwasababu ya bendera yake au sera zake? Hamad Rashi analo jibu!
 
Back
Top Bottom