PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Mgombea urais wa Chama cha ADC visiwani Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, ameahidi kupunguza gharama za mchele maarufu wa Mapembe endapo Wazanzibari watamchagua kuwa rais.
Amesema kuwa moja ya vipaumbele vyake ni kuhakikisha "mchele wa Mapembe" unapatikana kwa bei nafuu ya shilingi 1,200 za Kitanzania, ikilinganishwa na bei ya sasa ya takriban shilingi 3,500.
Kwa mujibu wa Hamad Rashid, hatua hiyo inalenga kupunguza mzigo wa maisha kwa wananchi wa Zanzibar, hasa wale wa kipato cha chini.
Hata hivyo, ahadi yake hiyo imeibua mjadala kuhusu uhalisia wa utekelezaji wake, ikizingatiwa hali ya uchumi wa sasa, gharama za uagizaji wa bidhaa kutoka nje na mabadiliko ya bei katika soko la kimataifa.