Hamad Masoud Hamad, ametangaza kujiondoa ACT Wazalendo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
1644394890654.png

ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, Hamad Masoud Hamad, ametangaza kujiondoa katka chama hicho.

Hamad ambaye aligombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa na kukosa nafasi hiyo, amefanya uamuzi huo akidai sababu ni chama hakina demokrasia.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Mjini Zanzibar, kuhusu uamuzi wake, alisema uchaguzi wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni, mkoani Dar es Salaam haukuwa huru na haki.

"Nilichokibaini katika uchaguzi mkuu wa uliofanyika, chama kilikuwa na mgombea wake maalum ambaye kilimuunga mkono," alidai.
Alieleza kuwa katika chaguzi zote za vyama vitatu alivyowahi kuwa mwanachama vya CCM na CUF wajumbe wote wa mkutano mkuu hawakuwa wakimpigia kampeni mgombea maalum badala yake huachiwa kupiga kura kwa mgombea wanayemtaka.

Alidai katika uchaguzi huo wajumbe walilazimishwa kumchagua Juma Duni Haji, na kwamba ni kinyume cha taratibu za uchaguzi.
Hamad licha ya kujitoa katika chama hicho lakini hajaweka msimamo wake kuhusu chama gani atakachojiunga nacho, ingawa kuna taarifa zisizothibitishwa kuwa kuna chama atajiunga nacho.

"Nimeshafuatwa kujiunga na vyama zaidi ya saba, lakini bado sijaamua chama gani nitajiunga," alisema Hamad.
Alidai kuwa awali wapenzi wengi wa Chama cha CUF waliojiunga na ACT - Wazalendo walikuwa na imani kwamba ni chama chenye kuleta mabadiliko, lakini kumbe ni chama cha watu wachache.

Aidha, alisema hakujitoa katika chama hicho kwa sababu ya kukosa nafasi ya uenyekiti, bali ni maamuzi yake baada ya kuona chama hicho hakiendeshwi kwa ukweli na uwazi.

Alisema haoni sababu ya aliyekuwa makamu mwenyekiti Zanzibar Juma Duni Haji kugombea nafasi ya uenyekiti kwa vile nafasi yake ya awali ilikuwa ikimpa nafasi ya kushiriki vikao vyote vya ndani ya chama hicho.

Alisema baadhi ya watu wanaimani kuwa atafilisika kisiasa kutokana na uamuzi wa kujitoa katika chama, lakini anaamini kuwa uamuzi wake huo ni kupiga hatua moja ya kujitangaza kisiasa.

"Japo sijaandika barua rasmi ya kujiengua katika chama, lakini ibaki kuwa kauli yangu hii inatosha kukihama chama hicho,” alisema.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu ACT-Wazalendo Zanzibar, Salum Bimani, alisema uchaguzi uliofanyika ndani ya chama mwezi uliopita wa kumpata Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ulifanyika kwa huru na haki na kabla ya uchaguzi huo kufanyika ulitoa fursa kwa kila mwanachama kuchukua fomu na kila mgombea kunadi sera zake mbele ya vyombo vya habari.

Alisema ni vyema Hamad akukubali kwamba kura hazikutosha kupata nafasi hiyo dhidi ya mgombea mwenzake Juma Duni Haji na chama kilitoa nafasi kwa mtu kufuata taratibu za kukata rufani kama hakuridhika na matokeo.

Alimpongeza mwanachama huyo kwa kutumia demokrasia yake ya kutoka ndani ya chama na kumtakia safari njema huko aendako.

pia soma:

Chanzo: Nipashe
 
Chama cha Zitto hakina demokrasia
 
Zito anaacha nyumba yake mlango wazi then anaenda kulinda mlango wa jirani yake kama sio unafiki ni nini.
 
angeshinda uchaguzi, chama ndio kingekuwa na demokrasia..!
 
Zitto hana sifa za kuongoza chama makini,ACT Wazelendo haina tofauti na TLP.

Bahati mbaya Zitto hajui kila mpango na mienendo yake inamvua nguo kila uchao.
 
Pamoja na mgogoro uliokuwapo CUF ,ndoa ya CUF na ACT ni sawa na ndoa ya TANU na ASP . Wazanzibari short changed again. Which way forward? CUF RELOADED bila shaka.
 
Back
Top Bottom