hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,448
Mke wangu amesajili laini ya halotel hizo wanazoita mpya (ilikuwa ni mwezi wa 3 kama sikosei). Laini hiyo ina PIN ya 0000 wakati wa kuwasha ambapo namba hiyo haibadilishiki (udhaifu mwingine huo ambao ni kero pia japo muda huu sijakusudia kuiongelea yenyewe)
Sasa hiyo laini imekuwa ikipokea sms za kunadiwa mavitu ya ajabu ajabu (wanaita ofa mbalimbali) ambapo kwa siku (ndani ya saa 24) zinafikia sms tano kwa wastani
Swala hilo mke wangu alinifikishia nikasema nimsaidie kwa kupiga huduma kwa wateja namba 100. Nilipopiga simu ile kupokelewa ilikuwa ng'anga na machekecho na hata ilipopokelewa niliambiwa tu "ngoja tulishughulikie tatizo lako"
Ilichukua siku kadhaa sms zinaingia kama kawa haoni mabadiliko ndipo nikapiga tena wakasema kuna huduma amejiunga nilivyomtolea hoja conc. akasema basi hiyo hajajiunga kitu chochote ila wataiondoa nisijali
Zikakata siku kadhaa tena ni vilevile nilipopiga huduma kwa wateja asante kwa kusubiri asante kwa kusubiri halafu kimyaa mpaka simu inakata mara kama ya tatu hivi likapokea likaka sijui libaba aisee nilijuta kupoteza muda wangu. (Hii ya mwanaume kukutana na kero akipokea kidume mwenzake huduma kwa wateja ni shida nyingine japo nayo pia sijaikusudia kuieleza hapa)
Lijamaa lilipokea halafu kauzu kinoma eti limenambia "nakusikiliza" basi nikaelezea tangu nilivyowasiliana nao mwanzo mpaka! Likauliza kama kuna makato yoyote nikanijibu hakuna eti sasa hukatwi unasumbukia nini nikalijibu sasa meseji zimezidi nataka muondoe likawa limenyamaza nilipoitika 'hallo' likanijibu kiukali "kata simu ili tuweze kushughulikia tatizo lako" nikakomaa kutaka kujua ni muda gani wangeshulikia maana siyo mara ya kwanza kuambiwa maneno hayo likaendeleza ukali na ukauzu wake eti "wewe si umeshalifikisha tatizo na nimekujibu litashughulikiwa tena...!?
Dah yaani nilikasirika nilipofikiria muda nilioutumia kungoja wapokee simu na mssaada wenyewe (huduma mbovu) nilopatiwa basi nikatamani nimtusi jamaa ila nikajizuia kisha kwa hasira nikadang'uza tu kisha nikakata simu -(kudang'uza sijui kiswahili kingine wanaitaje)
Hasira zote nikasema namalizia kwenye laini na mmiliki wake nikamwambia aivunje atupe huko (tena nilianza kumwambia hivyo tangu nilipopiga simu mara ya kwanza na hakuna msaada) naye kaing'ang'ania kweli hiyo laini basi nikamwambia "usiniombe msaada wowote kuhusu lilaini lako la halotel wala mimi silisevu linamba lako humu"
Mke naye anavyoniaminiaga kwenye maswala ya simu lakini katika hili tayari halotel mmesababisha nishuke hadhi kwa mke wangu dah!!! Ishala itala!
Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app