Habari wana jukwaa
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza tarehe 29/1/2022 nilikua nahamisha pesa kutoka halotel kwenda mtandao mwingine kwa bahati mbaya nikawa nimekosea kuhamisha ile pesa nikaamua kuwapigia nilipiga cm zaidi ya mara4 na haikupokelewa baada ya muda mfupi nikatumiwa ujumbe kua muhamara nilio fanya umefail kesho yake tarehe 30 nikapiga cm wakapokea wakanambia tatizo langu wameripot kwahyo wanashughulikia ndani ya masaa 24 nikasema sawa leo tarehe 1 nimepiga cm naambiwa tatizo linashughulikiwa kwahyo ningoje mpaka tarehe 3 ndipo pesa yangu itaweza kuludi swali ni je kama pesa ya mteja ilikua kwenye biashara na kama mnavyojua pesa ya biashara inakua kwenye mzunguko yaani ningoje zaidi ya siku5 ndipo pesa ije je biashara yangu inakua imeathirika kwa kiwango gani .
Pia kwanini mnakua hampokei cm kwa wakati yaani unaweza piga zaidi ya mara 5 na cm isipokelewe tena nyakati za usiku ndo unaweza piga hata mara 10 na wasipokee cm huku mitandao mingine watoa huduma wanakuepo masaa24[emoji35]