Halmashauri yamuadhibu diwani wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halmashauri yamuadhibu diwani wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ms Judith, Apr 21, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Halmashauri yamuadhibu diwani wa CHADEMA


  na Julieth Mkireri, Kibaha


  HALMASHAURI ya mji wa Kibaha Mkoani Pwani imetoa siku saba kwa Diwani wa Kata ya Tumbi kwa tiketi cha CHADEMA, Rajabu Makala, kuandika barua ya kuomba msamaha akidaiwa kutumia lugha ya kejeli kwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Adhudad Mkomambo, wakati wa kikao cha kupitisha bajeti ya mwaka 2011/2012.
  Maamuzi hayo yalifikiwa juzi baada ya diwani huyo kushindwa kuomba msamaha wakati alipohitajika kufanya hivyo na wajumbe wa baraza hilo ambalo pia lilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba.
  Akichangia hoja katika baraza hilo, Makala alitoa kauli ya kumwita mwenyekiti huyo kuwa ana ghiliba na ambaye anapendelea miradi ya maendeleo katika kata za madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuziacha kata za wapinzani zikiambulia kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
  Hata hivyo kauli hiyo ilipingwa vikali na mwenyekiti huyo kwa kusema kuwa yeye ni mwenyekiti wa madiwani wote na hayupo kwa ajili ya kupendelea baadhi ya kata zinazoongozwa na madiwani wa chama chake.
  "Mimi ni mwenyekiti wa madiwani wote na siko kwa ajili ya kupendelea kata fulani, kuingia kwangu kwenye kila kamati ya madiwani ni kwa mujibu wa kanuni na pia ninatenda haki kwa kushirikiana na madiwani wote, sibagui kama unavyodhani hata wewe ukiniita kwenye kata yako ninakuja, tunajadili changamoto za kata yako," alisema Mkomambo.
  Makala aliendelea kulalama ndani ya kikao hicho cha bajeti juu ya wananchi wa kata yake kutotengewa fedha kwa ajili ya matengenezo ya kawaida ya barabara na mambo mengine ya maendeleo ambayo aliyawasilisha katika halmashauri ili yaweze kupewa kipaumbele kwenye bajeti lakini haikufanyika kama ilivyotakiwa.
  Hata hivyo madiwani waliendelea kusimama mmoja baada ya mwingine wakimshawishi Makala kuomba msamaha ili kikao kiweze kuendelea lakini ilichukua muda zaidi ya nusu saa kufanya hivyo na hata hivyo hakuomba msamaha na kikao kiliendelea.
  Kutokana na kukaidi baraza lililazimika kutoa siku saba kwa Makala kuandika barua ya kuomba radhi na kama atashindwa kutii maamuzi hayo kanuni na taratibu za baraza zitachukua nafasi yake kwa kamati ya maadili kumweka chini kumjadili na wakati huo atalazimika kutohudhuria vikao viwili na kukosa posho zake katika vikao hivyo.
  Maamuzi hayo yalisababisha vuta ni kuvute baina ya wajumbe wa baraza hilo baadhi wakimshauri diwani huyo kuomba radhi na upande mwingine ukiruhusu taratibu za kimaadili zichukuliwe dhidi yake.
  Wakati mvutano huo ukiendelea, Mwenyekiti Mkomambo alisema kuwa awali kikao hicho kilipoanza Diwani Makala alilalamikia suala kutozingatia muda na kuomba kikao hicho cha bajeti kiahirishwe, jambo ambalo mwenyekiti huyo pamoja na mkurugenzi waliomba radhi na kikao kuendelea na kuhoji kuwa iweje yeye ashindwe kuomba radhi pale anapobainika kukosea?
  Naye Mkuu wa wilaya hiyo, Halima Kihemba, alikemea tabia ya baadhi ya madiwani hao kurushiana maneno yasiyo na msingi katika vikao kwani kwa kufanya hivyo ni kurudisha nyuma malengo ya vikao vya halmashauri na jitihada zake za kuweka mikakati ya kukuza mji huo.
  Hatua hiyo ilimsukuma mwandishi wa habari hizi kumtafuta kwa njia ya simu Diwani Makala kuhusiana na maamuzi ya kikao na bila wasiwasi alipaisha sauti yake kuwa hatathubutu kuandika barua hiyo kwani mwenyekiti wa halmashauri hiyo amewahi kumtolea kauli zisizo za kupendeza ndani ya kikao hicho kwa kumuita mhuni, lakini hakuombwa msamaha, hivyo na yeye hawezi kuomba msamaha.
  Sambamba na hayo, Halmashauri ya Kibaha Mjini imepitisha zaidi ya sh bilioni 14 ikiwa ni bajeti yake ya mwaka 2011-2012, huku madiwani wa Kata ya Tumbi na Msangani wakitoa malalamiko yao juu ya kamati ya fedha kutokuwa na mgawanyo sawa wa fedha za miradi katika kata zote.


  source:
  Halmashauri yamuadhibu diwani wa CHADEMA
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  halima kihemba kwanini unaingilia vikao vya wawakilishi wa watu?? wewe unamwakilisha nani aliyepo ktk halmashauri ya kibaha, wewe umeteuliwa tu kwahiyo unawajibika kwa yule aliyekuteua na siyo kwa wanannchi wa kibaha. wacha maamuzi ya watu wa kibaha yafanywe na watu wa kibaha na siyo kuingilia vikao vya baraza la wananchi wakati hakuna mwananchi hata mmoja anaweza kuku hold accountable unapoaribu kazi lakini madiwani hao wananwajibika kwa wananchi waliowachagua.
   
Loading...