Halmashauri ya Wilaya Geita na Mchezo Mchafu Katoro

Halmashauri ya Wilaya Geita na Mchezo Mchafu Katoro

Mshangai

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2008
Posts
468
Reaction score
1,087
Mji mdogo wa Katoro ndio nyumbani kwetu. Siku mbili tatu zilizopita nilikuwa nyumbani kwa masuala ya kifamilia, na katika pitapita yangu nikawaona vijana walioniambia kuwa ni Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Ardhi Dar es Salaam wakiwa wanazunguka mitaani na jua kali wakifanya kazi ya kutengeneza MASTER PLAN ya mji huo ambao nimeambiwa unakuja kugeuzwa kuwa makao makuu ya wilaya ya Geita. Ni mpango mzuri kwa faida ya wilaya yetu na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo baada ya kuzungumza na watendaji wawili watatu wa serikali za mitaa hapo Katoro nimesikitishwa sana na niliyosikia.

Serikali pamoja na kutenga fedha za mradi huo, haijapeleka pesa yeyote kugharamia kazi hiyo, wanachofanya ni kutumia vijana hao walioko field kama kazi ya bure.

Na kwa vile Wanafunzi hao hawajui maeneo na wanapaswa kuwa na wenyeji (watendaji) ambao wamegoma kufanya kazi bure inawapasa Wanafunzi hao wawalipe posho watendaji hao shs 10,000/ kwa siku ili kazi assignment zao zisilale kulingana na muda. DHULUMA YA AINA GANI HII?

Ni kweli kuwa wnafunzi wanapewa tuposho twa kujikimu wawapo field lakini ni sawa kwa wao kuwalipa watendaji ili kazi yao iliyowapeleka huko ifanikiwe? Pia kati ya wanafunzi hao wapo ambao hawapo kwenye scheme ya kupewa mikopo na wanadhaminiwa na wazazi wao kila kitu jee ni halali serikali kuruhusu jamabo hilo?

Mkurugunzi Mtendaji wa Halmashauri ya Geita anafahamu umuhimu wa kazi hiyo, DC naye pia, Afisa mipango wa H/w naye yupo kweli hawa ni watendaji wa aina gani wanashindwa kuliona hilo na kuchukuwa hatua?

Hivi kazi hiyo inaweza kufanyika kwa umakini kama hali ni ya aina hiyo? Nadhani wanaruhusu uwepo ulipuaji wa kazi kwa vile wao kesho na kesho kutwa wanaweza kuwa wamehama na yatakuwa hayawahusu.

Halmashauri ya wilaya hebu oneni umuhimu wa kazi hiyo,hata kama mumeipata kama free labour lakini ni ya kitaalamu haipaswi kufanywa katika mazingira ya kimasikini na taabu wakati pesa imetengwa au ipo kidogo. Vinginevyo watu wawajibishwe maana wao wataondoka na Katoro yetu itaendelea kuwepo.
 
Habari mpya ni kuwa Watendaji wa kata wameweka mgomo baridi kama wataendelea kulipwa na wanafunzi badala ya kulipwa na Halmashauri kwani wanaona wanadhalilika.
Tamisemi waingilie swala hili la sivyo kutakuwa na mpango mji usio elewka kwa Katoro na mji wetu unakuwa kwa kasi.
 
Eee mungu wasaidie vujana hawa wasiwe na visasi wapatapo kazi serikalini.kwa kuiba serikalini kulipiza taabu na dhuruma wanazozipata saivi.
 
Katoro haiwezi kuwa makao makuu ya wilaya geita kuwa makao ya wilaya hiyo yako geita mjini,labda kukianzishwa wilaya mpya ya busanda.
 
Katoro haiwezi kuwa makao makuu ya wilaya geita kuwa makao ya wilaya hiyo yako geita mjini,labda kukianzishwa wilaya mpya ya busanda.

Ninavyofahamu mie ni kuwa Makao makuu ya Wilaya ya Geita yanataka kuhamishwa kutoka Geita mjini ili pabaki kuwa makao makuu ya mkoa.
Sasa tatizo ndio hilo kwamba kila mradi mpya watu wanataka kufanya mambo ya ulaji bila kujali wengine. Hofu yangu ni wale vijana katika hali ya shida kweli watafanya kazi hiyo kwa umahiri au ndiyo yale ya kanyaga twende na Mkurugenzi na wengine wanaona safi tuu kwa vile wao sio wazawa na ya mbele hayawahusu?
 
Kuna wajanja wamepiga hio pesa wanasingizia haijaletwa toka serikalini.
Kwakuwa hao wanafunzi wanafanya field, wameamua kuwatumia bure.
ni dhuluma mbaya sana.
 
Back
Top Bottom