Halmashauri ya Kinondoni yapata tuzo ya Halmashauri bora Afrika

Halmashauri ya Kinondoni yapata tuzo ya Halmashauri bora Afrika

purtpurt

Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
38
Reaction score
6
Channel 10 TV - hapa naona Halmashauri ya Kinondoni inapokea zawadi ya kuwa Halmashauri bora Barani Afrika. Loh. Kumbe na sisi tupo! Mungu endelea kuibariki Tanzania!!
 
Sijaelewa wamepata tuzo hiyo kwa kufikia vigezo gani lakini pamoja na mambo mengine nadhani inaweza kuwa ni kutokana na perfomance nzuri kwa mambo mengi ikiwemo kuongezeka kwa mapato isivyo kawaida kulinganisha na huko nyuma.

Kudos kwa madiwani na wabunge wa upinzani kusaidia kuziba mianya ya wizi na ubakaji mapato ya halmashauri kuliko kuwa kunafanywa na genge la viongozi wa CCM na mawakala wao.
 
Pongezi ziende kwa hasa madiwani kwani wange kuwa ndio ndio wasinge fikia malengo
 
Sijaelewa wamepata tuzo hiyo kwa kufikia vigezo gani lakini pamoja na mambo mengine nadhani inaweza kuwa ni kutokana na perfomance nzuri kwa mambo mengi ikiwemo kuongezeka kwa mapato isivyo kawaida kulinganisha na huko nyuma.

Kudos kwa madiwani na wabunge wa upinzani kusaidia kuziba mianya ya wizi na ubakaji mapato ya halmashauri kuliko kuwa kunafanywa na genge la viongozi wa CCM na mawakala wao.

Na hilo pia linachangia kwa % kubwa
 
Hapa nimekuwa na mashaka makubwa ni hii tuzo! Huenda kuna asilimia kubwa wametoa rushwa kuipata! Huwezi kusema kigezo ni kituo cha simu2000 kituo kilichopo sehemu isiyo na barabara ya kuingilia! Kimepoteza hata ustaarabu wa wana dar kipindi hiki cha mvua
 
Channel 10 TV - hapa naona Halmashauri ya Kinondoni inapokea zawadi ya kuwa Halmashauri bora Barani Afrika. Loh. Kumbe na sisi tupo! Mungu endelea kuibariki Tanzania!!

Halmashauri bora barani Afrika?! Kweli...!!!!? Mambo mengine ni dhihaka tupu, tena dhihaka hasa. Jana nilipoona kwenye taarifa ya habari nilibaki na mshangao... Hebu tujifikirishe kidogo
-mshindanishaji alikuwa ni nani?
-Alitumia vigezo gani muhimu!?
-Alitumia halmashauri za majiji mangapi yenye mfumo kama wetu?

Kwa miundombinu ile ya kuingilia na kutokea halafu kinondoni ikashika no 1, sijui aliyeshika mkia yukoje? Najua tunapenda mno maigizo lakini yasiachane mno na uhalisia
 
Tujifunze kujitambua na kufanya utafiti japo kidogo. Manispaa ya Kinondoni imejitahidi kufanya mambo mengi kwa kutumia fedha zake. Imeongeza ukusanyaji wa mapato. Meya wa manispaa hii ni kijana msomi na makini. Tuzo hizi ni kwa miji inayokua kwa kiwango cha kati na siyo majiji.
 
Labda tuzo ya kuwa manispaa chafu kuliko zote ulimwenguni.
 
Halmashauri bora barani Afrika?! Kweli...!!!!? Mambo mengine ni dhihaka tupu, tena dhihaka hasa. Jana nilipoona kwenye taarifa ya habari nilibaki na mshangao... Hebu tujifikirishe kidogo
-mshindanishaji alikuwa ni nani?
-Alitumia vigezo gani muhimu!?
-Alitumia halmashauri za majiji mangapi yenye mfumo kama wetu?

Kwa miundombinu ile ya kuingilia na kutokea halafu kinondoni ikashika no 1, sijui aliyeshika mkia yukoje? Najua tunapenda mno maigizo lakini yasiachane mno na uhalisia

Kuna jambo halikufafanuliwa vizuri nadhani.Sıdhani kama mfumo wa ugatuzi unafanana nchi zote.Alafu baadhi ya nchi ziko centralized kwa kıla jambo.Labda kwa nchi zenye utaratibu wa kiutawala kupitia hzo halmashauri ndo yaweza kuongoza.
 
Hawakutoa tuzo ya tz ya pili kwa utajiri barani Afrika? Tunapenda tuzo bila uhalisia uliopo.
 
Watanzania wachawi, hawaipendi Tanzania. Jamani hii ni nchi yenu ulizaliwa hapa na utafia hapa. Ipende hata kinafiki
 
Watanzania wachawi, hawaipendi Tanzania. Jamani hii ni nchi yenu ulizaliwa hapa na utafia hapa. Ipende hata kinafiki
Root naipenda sana nchi yangu tena sana lakini siwezi kuwa mnafiki penye ukweli nyeusi nitaita nyeusi
 
Last edited by a moderator:
Watanzania wachawi, hawaipendi Tanzania. Jamani hii ni nchi yenu ulizaliwa hapa na utafia hapa. Ipende hata kinafiki

kupenda kitu hakimaanishi uwe mnafiki kwa kusema uongo ktk kitu halisi kilichopo. Naipenda sana Tanzania sana lakini kwa kusema kuna ka sehemu ya jiji la Dar wamepata tuzo ya Afrika huo ni UJINGA.
 
Watanzania wa ajabu sana (hasa wachadema). Hata likitokea zuri kwao hawapongezi wanasubiri baya waponde
 
ImageUploadedByJamiiForums1430976749.444263.jpg ImageUploadedByJamiiForums1430976771.636381.jpg
 
Back
Top Bottom