MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Kwa mtufuano unaoendelea kuna uwezekano mkubwa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuvunjwa na kubakia mikononi mwa Serikali Kuu chini ya usimamizi wa Ofisi ya Rais, Wizara ya Tamisemi.
Kigezo kitakachotumika ni kushindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi kwa sababu ya vurugu na upungufu wa akidi ndani ya vikao vya Madiwani.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam,. Mwaka 1996 tulishuhudia Waziri Mkuu, Frederick Sumaye akilivunja Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam lililokuwa likiongozwa na Meya, Kitwana Kondo na kuunda Tume iliyokuwa chini ya aliyepata kuwa Mbunge wa Ubungo, Charles Keenja.
Baada ya Baraza la Madiwani kuvunjwa, makusanyo yalipanda mpaka Sh9 bilioni kutoka kama sh900 milioni.
Sehemu ya Kanuni za kudumu za Mamlaka ya Miji kuhusu akidi zinasema,
9 (1) Hakuna Mkutano wa kawaida wa Halmashauri utakaofanyika isipokuwa kama utakuwepo idadi ya Wajumbe isiyopungua nusu ya Wajumbe wote waliohudhuria na kujiandikisha kwenye daftari la mahudhurio.
(2) Akidi katika Mikutano maalum ya Halmashauri itakuwa ni theluthi mbili ya Wajumbe wote wa Halmashauri na itahesabiwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano.
(3) Akidi katika Mkutano wa kawaida wa mwaka na Mkutano wa kwanza wa Halmashauri itakuwa theluthi mbili ya Wajumbe wote wa Halmashauri.
(4) Endapo Wajumbe waliohudhuria Mkutano hawatafikia akidi ya Mkutano, Mkurugenzi atauahirisha Mkutano huo na kuitisha tena ndani ya siku saba (7) na endapo akidi haitatimia tena, idadi yoyote ya Wajumbe waliohudhuria itatengeneza akidi ya Mkutano na Mkurugenzi atamjulisha Waziri kuwepo kwa hali hiyo.