Halmashauri ya Jiji la Arusha inatetea mafisadi/madalali

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Kweli jiji la Arusha linazalisha maajabu kila kukicha.
Hivi sasa wametangaza tenda ya kupangisha maduka yake ambayo tayari yana wapangaji wenye leseni hai walizotoa wenyewe.

Mwaka jana waliwasainisha hao wapangaji mikataba ya upangishaji ambayo sasa wamekataa kuwapatia.

Wamewapa notisi wapangaji eti kwa kutumia sheria ya manunuzi wakati upangishaji wa majengo unatawaliwa na sheria za ardhi.

Wanafanya haya yote kwa sababu za kisiasa kwani kuna mafisadi/madalali waliokuwa wapangaji ambao waliwapangishia watu wengine maduka yao kwa kodi kubwa- zaidi ya mara tatu ya kodi waliyokuwa wakiilipa halmashauri. Wengi wa mafisadi hao ni wanachama wa CCM.

Halmashauri ilipofanya sensa ya maduka yake ikagundua hiyo kasoro na kuwahalalishia upangaji wafanyabiashara waliokuwa ndani ya maduka hayo ambao walikuwa na leseni za biashara.

Kwa kuwa kwa sasa halmashauri inatawaliwa na Chadema hao wana CCM walilalamika kwa mamlaka za juu kuwa wamenyang'anywa kwa sababau za itikadi zao za kisiasa.
Kwa mshangao mamlaka hizo zimeagiza upingashaji ufanywe upya kwa kutangaza tenda ili kila mwenye uwezo aombe pamoja na hao mafisadi/ madalali.

Tunaomba haki itendeke kwa (a) Mikataba iliyowekwa sahihi itolewe badala ya kuingizia wapangaji gharama nyingine za tenda na mikataba mipya kwani tenda kama ni lazima itumike tu kwa majengo mapya au yaliyo wazi na hayana wapangaji.

(b) Hao madalali wasituharibie uhusiano wetu na halmshauri kwani faida waliyopata kwenye huo udalali ambao ni kinyume cha sheria inawatosha.
 
Mstahiki Meya Kalisti Lazaro hujaona hii? Tumia mamlaka yako kufuta hiyo tenda au toa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom