Halmashauri - Mrema huyo anakuja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halmashauri - Mrema huyo anakuja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jenifa, Mar 7, 2011.

 1. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  baba daktari mrema akisema hutekeleza

  Wabunge kuwaweka 'kiti moto' watendaji halmashauri

  Daniel Mjema, Same
  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) leo inaanza ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro ambapo inatarajiwa kuwaweka kiti moto baadhi ya watendaji wa halmashauri kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Umma.

  Ziara hiyo inafanyika kipindi ambapo Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akiwa ametoa taarifa ya ukaguzi maalumu uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo iliyobaini ufisadi wa zaidi ya Sh914 milioni.

  Mwenyekiti wa LAAC ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo,Agustine Mrema (TLP) alitahadharisha kuwa katika ziara hiyo hakutakuwa na msalie mtume wala kulindana na watataka maelezo kuhusu utekelezaji wa maagizo ya CAG.

  "Hii ziara, lengo lake mahsusi ni kufuatilia utekelezaji wa ripoti ya CAG, tunataka kujua kama kuna watu walitakiwa kuwajibishwa wamewajibishwa na je polisi na Takukuru wamechukua hatua zipi baada ya ripoti hizo,"alisema Mrema.

  Mwenyekiti huyo alisema "kesho (leo) tutaanza na Same na baadaye Mwanga na wilaya zingine za mkoa Kilimanjaro na tutapitia halmashauri zote nchini na tutagusa kila mahali".

  Mrema alizitaja wilaya watakazozitembelea kuwa ni Same, Mwanga, Rombo na Moshi Vijijini na kuonya kuwa kama serikali haitajipanga vizuri kukabili wizi aliodai ni wa kutisha kwa baadhi ya Halmashauri basi hakutakuwa na maendeleo.

  "Rais Kikwete na serikali yake wananatuma pesa nyingi sana kwenye halmashauri, lakini tatizo ni ufisadi wa baadhi ya watendaji, wanazitafuna kama mchwa tumesema sasa imetosha,"alisema Mrema.

  Mrema alifafanua kuwa fedha zinazotumwa kwenye halmashauri kwa ajili ya miradi ya maji, kilimo,afya na ujenzi wa barabara ni mabilioni ya shilingi, lakini kazi zilizofanywa hazilingani na fedha zinazoonyeshwa kutumika.

  Mwenyekiti huyo aliiomba Serikali kufanya maamuzi magumu ya kuwafukuza watumishi wote wa halmashauri wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi na ubadhirifu vinginevyo suala la maendeleo litakuwa ni ndoto kwa wananchi.

  Ziara ya kamati hiyo imekuja wakati Mbunge wa Jimbo la Rombo, Joseph Selasini akiwa amemuomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuingilia kati sakata la ufisadi wa Sh 914 milioni unaodaiwa kufanywa na watumishi 12 wa halmashauri.

  Katika barua yake ya Februari 14, aliyomwandikia Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), mbunge huyo alilalamikia kitendo cha mkuu wa wilaya kusimama upande wa watuhumiwa.

  Selasini katika barua hiyo ambayo Mwananchi imeiona alilalamika kuwa mkuu huyo wa wilaya kama mwakilishi wa Rais alipaswa kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kupambana na maovu katika jamii ikiwamo ufisadi.
   
 2. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa zimechelewa sana. Ilitakiwa tangu wakati huo magugu yote yawe yametolewa shambani hata kama ni huyo mkuu wa Wilaya n.k. Tuone kinachofuata isiwe longolongo ---tumechoka kusikia blah blah...
   
Loading...