GE2025 Halima White: Kwa vyovyote vile Rais Samia atashinda uchaguzi mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na pia Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma, Ndugu Halima White Zuberi, amesema kuwa kwa mshikamano wa wakazi wa Dodoma na wanachama wa CCM, watahakikisha chama hicho kinapata ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Zuberi ameyasema hayo leo, Jumatano Julai 2, 2025, jijini Dodoma aliporejesha fomu ya kuwania Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Dodoma.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesema kuwa wanachama wa CCM watafanya kila jitihada kuhakikisha wanazipata kura zote za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wote wa CCM wanaotegemea kuteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo Madiwani na Wabunge.

"Chama chetu kitaendelea kuwa ngome imara katika Mkoa wa Dodoma, na sisi kama wanachama tutahakikisha hilo linafanikiwa, iwe inanyesha mvua ama jua linawaka," amesema Zuberi kwa msisitizo.

Your browser is not able to display this video.
 
Another neck supporting an empty coconut 🥥 head.
 
Reactions: 004
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…