Halima Mdee Yupo Juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halima Mdee Yupo Juu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamanzi, Feb 9, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Asalam Aleikum waungwana. Kwa mara ya kwanza nimemuona kwenye clip kamanda Mdee akimwaga hoja bungeni na I must admit huyu dada yupo makini. Ni kweli machache nijuayo kuhusu yeye najua kwamba ana masters ya laws lakini kuongea kwa ujasiri namna vile huku amezungukwa na wanyonya damu mbumbumbu zaidi ya 200 toka CCM, wabunge wafu kadhaa toka CUF na vibaraka wengine toka NCCR, TLP na UDP si mchezo. Kwa mtazamo wangu, yupo juu zaidi ya Zitto na Mnyika. Kwamba ni yeye binti ni bonus nyingine. NA zaidi nafurahi kuwa ni binti msomi wa kiislamu amabe nina uhakika kwa miaka mingi ijayo atakuwa taa ya kuonyesha njia waislamu kwa wakristo mpaka waje kula mema ya nchi yao siku moja. Atakae muoa huyu, atakuwa ame-hit jack pot.
   
 2. Mhubiri

  Mhubiri Senior Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  muombe ukanywe nae chai
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,060
  Trophy Points: 280
  Kwa msomaji aliye makini atagundua mambo unayotaka yajadiliwe si Halima Mdee yuko juu believe me or not.
   
 4. v

  vickitah Senior Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hasa ni nini kimekugusa mkuu weka hadharani mkuu' nakubaliana na wew ni binti anayejiamini.. nimemskia akimtwanga maswali yule jamaa wa maji pale nikaguswa zaidi' ila naona suala la kumfananisha na Zito na Mnyika ni gumu kwa upande wangu maana nadhani wote ni makini na sidhani km Mdee naweza kusema amewapita au lah!

  Kwa kifupi CDM ipo kamili.. nadhani hata arguments za wanachama wao pia zinathibitisha hilo'
   
 5. M

  Mndamba Namba 1 Senior Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halima Yuko vizuri,na CDM kwa ujumla la kuhusu yeye ni binti wa kiislamu sina uhakika mana nijuavyo yeye ni Halima James Mdee jina la halima alichukua la bibi yake,wanaojua dini yake vizuri watusaidie sio kwa lengo la kuleta udini la hasha ila kwa ajili ya kuwa na mtiririko mzuri wa ufahamu wa huyu mwanadada jasiri
   
 6. k

  kamanzi Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Quinine unataka kuzua majungu kwenye jambo ambalo halina ubishi. Mimi namzungumzia Halima kama mtu jasiri mwenye vigezo. Lipi unalosema nataka lizungumzwe zaidi ya hapo. Wewe ulisikia/uliona kelele zilizokuwa zikipigwa wakati akiongea? Kwa mfumo wa kitanzania ambao wanawake wengi wanaingia kwa viti maalumu sidhani kama ninakosea nikisema binti akiwa na ujasiri kama vile ni tunu. Au kwasababu nimesema ni mjuislamu? Mimi nakiri simfahamu na zaidi ni kwamba naishi nje ya nchi na mpango wa kurudi sina kwaiyo nikama haiwezekani kukutana nae kama ulifika huko nako. LEt's face it, kwa level ya Tanzania, huyu dada yupo juu mno. KWanini nasema yupo juu zaidi,. Ni kwasababu kwenye affirmative action policies mwanamke akiwa at least level na mwanamme, advantage inakuwa kwake. KWani ndugu yangu Quinine dada yako alipokuwa akipika jikoni na kuosha vyombo ulikuwa unamsaidia? Iweje wote mkipata masters muwekwe fungu moja wakati wewe ki-Tanzania ni mwanamme hivyo kazi za ndani hufanyi?
   
 7. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwani kila kitu lazima kijadiliwe hapa?:twitch:
   
 8. S

  Selemani JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ofkoz mbunge wangu Halima Mdee yuko juu. Huwezi kumlinganisha na puppet wa Mbowe Mnyika, au mpenda masifa Zitto. As the matter of fact apart from Slaa, the only asset in that party is Halima Mdee. She just need to be more independent off Mbowe eraticism and less pampous like Tundu Lissu.
   
 9. c

  chumakipate Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ningefurahi kama ungetumia maneno binti msomi wa kitanzania(sio wa kiisilam)...after all:Maisha Binafsi Halima James Mdee alizaliwa katika familia ya Wakristo na alibatizwa na kuitwa Theodosia, hata hivyo anatumia zaidi jina alilorithi kutoka kwa bibi yake mzaa baba, Halima.
  Ukoo wake ni waumini wa dini ya Kiislamu isipokuwa baba yake na kaka yake ambao walibatizwa na familia yao ikaridhia wawe Wakatoliki. ifakara..soma wikipedia
   
 10. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Halima mdee sio muislam banaa musituongopee hapa. Kama ujasiri ni kutukana watu na kuongopa basi kweli halima ni jasiri lkn kama sio hivyo mimi sijamuona hata kimoja cha maana alichokisema hata wabunge wenzake walimwambia kua hana hoja kazoea mipasho. Namshukuru spika kwa kumueka sawa pale alipotaka kupotosha umma kwa kusema eti ile 12.5% iliekwa mwaka 2007. Akabakia kutoa mdomo kama nyani.
   
 11. k

  kamanzi Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ni kweli ndugu yangu Chumakipate, the right wording ingekuwa binti msomi wa kitanzania, ila nilitamani kuwe na angle inayoonyesha kuwa kinyume na mitazamo ya CCM, waislamu wengi wanajitambua. Inawezekana huyu Halima ni mkristo ila natamani atokee muislamu halisi mwenye mitazamo kama hii. Upo wakati Zitto alikuwa na muelekeo lakini kamati ya JK ikamchakachua hadi leo hajaweza kuinuka tena toka kwenye anguko lake. Natamani wajitokeze ili mafisadi wa CCM waache kusema CHADEMA kinaudini.

  Sasa wewe Mtabe, kama Halima anatoa mipasho hao wazee wa CCM watakuwa vipi. Yaani mijitu yenye mvi inamzomea binti mdogo namna hiyo si aibu hii jamani. Walitakiwa ndio wamwonyeshe njia badala yake yeye ndio anawaonyesha. HIVI wapenda CCM kama wewe Mtabe nini mnachofurahia huko? Low lifers wote wapo huko, maskini hata wasomi nao wamekuwa kama wahuni tu maadamu wapo CCM. Brazameni Dr Dr Dr kawaambukiza ulofa kweli. YAngu macho mie!!!
   
 12. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi jana Halima Mdee alitoa point gani pale? kwa hoja zake zile kweli unaweza ukamtofautisha na Mama Sofia Simba? Kweli kipenda roho ula nyama mbichi!!
   
 13. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,599
  Likes Received: 2,983
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nawe kuwa Halima Mdee ni mbunge msomi aliyeelimika, kijana na jasiri, na anayeonekana kuwa thabiti kupambana na chama dhalimu CCM na wasaidizi wake kwa manufaa ya walio wengi ila hilo la kama ni muislam, mkristo au mpagani halina umuhimu, cha muhimu ni kuwa ni mtanzania mwenzetu anayepigania haki za walio wengi wanaodhulumiwa na utawala wa CCM.
   
 14. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  PHP:
  NA zaidi nafurahi kuwa ni binti msomi wa kiislamu amabe nina uhakika kwa miaka mingi ijayo atakuwa taa ya kuonyesha njia waislamu kwa wakristo mpaka waje kula mema ya nchi yao siku moja.
  Kwa kifupi hicho hapo juu ndo ulichotaka tujadili sivyo??? Imekula kwako mkubwa!!!!
   
 15. m

  matawi JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ulianza vizuri ulipoingiza ka udini nikahama jukwaa la siasa kwenda celebrities
   
 16. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  wewe kila kitu unakiangalia kwa jicho la udini tu? Hapo Tanzania ina hasara kubwa. Badilika ndugu yanu udini haujengi wala ukabila wala ubaguzi wa aina yoyote. Mpe sifa yake anayestahili na wenye hekima watakuuga mkono. Unapoleta hoja na kutia udini ndani yake unaharibu ladha ya thread. Peleka kwenye jamvi la kidini kama wewe hakieleweki isipokuwa dini kila wakati. Bora unyoofu wa moyo kulikodini unayoipigia upatu ambayo hata mbinguni hakuna dini inayompeleka mtu. Dini dini dini !!!!
   
 17. Mwadui

  Mwadui Senior Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  halima yuko juu na kuna sababu nyingi zinazomfanya kuwa juu,ikiwa elimu,malezi na kujiamini kuhusu uislamu sina uhakika kwana hata rais ni muislamu lakin bogaz hana anachoweza wala kujua,
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na kweli yupo juu kwa kuwa shakula cha wazee ! hongera mama
   
 19. R

  ROMAN REIGNS Member

  #19
  Jun 27, 2015
  Joined: Apr 24, 2015
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alima mdee ana miaka migapi
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2015
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Alima mdee ni jina la shangazi yako au? Au unamaanisha Halima Mdee.? Kama ninhuyu ana miaka 21
   
Loading...