Halima Mdee Unachemka

Halima Mdee Unachemka

dizbap

Senior Member
Joined
Nov 25, 2009
Posts
156
Reaction score
86
Hi Mh. Halima Mdee, ujue 2015 ndio hiyoo inakuja na sisi wananchi wa jimboni kwako tunakuangalia tu na promise zako ambazo unashindwa tekeleza. vitu vidogo vidogo tu vinakushinda sasa ukikosa hili jimbo lako utatulaumu?

Mwaka Jana mwezi kama wa Nne hivi kama si kosei tulikuita sisi wananchi wa Boko eneo la Magereza tena umekuja baada ya kukuita bila mafanikio kwa mara mingi, siku hiyo nakumbuka ukaja tukakutana na wewe pale Pommy Hill Club tukaongelea swala la Barabara yetu huku boko magereza. kwa Nyodo nyingi sana ukijifanya utashughulikia swala hilo na katika kile kikao ukawa mkali mkali tu,kikao kimeisha ukasema baada ya mwezi utarudi ilikutane na wamiliki wa magari yanayo beba mawe maana wao ndio wanao haribu barabara. na siku ile kuna mtu alisema wewe utuachie azimio kama baada ya huo mwezi hakuna lililofanyika tufunge barabara kwa magari makubwa ukakataa na ukasema utarudi yule mtu akarudia kusema " Nawajua wana siasa maneno mengi sana, naambia huyu harudi tena huku" na kweli alio yasema ndio yalio tokea.

Sasa angalia picha za barabara uliosema utarudi baada ya mwezi na sasa ni mwaka hatujakuona.
IMG-20140327-01221.jpg IMG-20140327-01224.jpg

Mimi napenda Mageuzi sana lakini jinsi hii itabidi CDM watupe mgombea mwingine jimbo hili wewe unachemka sana. una issue kama kumi hivi ushachemka sana kama CDM hawaoni basi hili Jimbo tutalikosa wakikusimamisha wewe tena.

Asante sana.
 
bi.josephin mushumbus atampokea halima mdee jimbo la kawe.. jiandaeni kumpokea first lady
Watuletee yoyote yule but awe mchapakazi tu. Huyu Sister do Mdee naona kesha kuwa Tajiri sasa amesahau Mapinduzi, Kawa Bepari a.k.a Magamba
 
Halima mda mwingi hushinda Saloon akijitumbua Chunusi sugu,huku akiwaza atazaa lini maana bado ni Single
 
Watuletee yoyote yule but awe mchapakazi tu. Huyu Sister do Mdee naona kesha kuwa Tajiri sasa amesahau Mapinduzi, Kawa Bepari a.k.a Magamba
utakuja kushangaa tena anatumia pesa kununua shahada kisha anakuwa mbunge tena!
 
Watuletee yoyote yule but awe mchapakazi tu. Huyu Sister do Mdee naona kesha kuwa Tajiri sasa amesahau Mapinduzi, Kawa Bepari a.k.a Magamba
Tatizo lake huyu binti ni kutokubali ushauri, ni mbishi sana hata sisi makamanda wenzake anatupasua vichwa, ilikuwa kazi ndogo kupanga ratiba ya kujichimbia jimboni kwa siku 10 ya kila mwezi, angefanya maajabu, lakini sijui yuko occupied na nini sijui wakati jimbo hili lina watu wenye kuwa tayari hata kujichangisha kuchonga barabara zao. Magamba hawaaminiwi kabisa na wanchi kukabidhiwa michango yao
 
Mdee achambue ushauri huu,asidharau na kuutupilia mbali.
Ndio maana tunasema wanasiasa wasitoe ahadi hewa,kama Chalinze nasikia Riz moko kaahi trekta kila kijiji na akishinda atakuwa na hardly mwaka mmoja tuu
 
mlio karibu na mheshimiwa Halima Mdee wajibikeni kwa kumfikishia Ujumbe kutoka kwa mwananchi. Mkiona haina mvuto ipotezeeni, ....Oktoba 2015 sio mbali.
 
Tatizo lake huyu binti ni kutokubali ushauri, ni mbishi sana hata sisi makamanda wenzake anatupasua vichwa, ilikuwa kazi ndogo kupanga ratiba ya kujichimbia jimboni kwa siku 10 ya kila mwezi, angefanya maajabu, lakini sijui yuko occupied na nini sijui wakati jimbo hili lina watu wenye kuwa tayari hata kujichangisha kuchonga barabara zao. Magamba hawaaminiwi kabisa na wanchi kukabidhiwa michango yao

Offcoz sisi hatutaki msaada wake yeye anatakiwa atu mobilize tu tufanye wenyewe.
 
Hatuwezi kumpa tena maana hata hatujui anafanya kazi gani!

Kwa kifupi ni hatumpi mtu yeyote wa CHADEMA kwasababu ni walaghai.

Tutampa Mh. Zitto kama itatokea akagombea vinginevyo ni CCM. Haturudii makosa kuwachagua hawa wachumia tumbo wa chama cha ukoo wa Mtei.
 
Mdee anakusanya kodi Kawe?
Hata kama hakusanyi Kodi Kawe ila yeye ndio Sauti yetu kwa Serikali. Sasa kama haongei habari zetu kwa serikali anaongea habari za nani? hili ni jukumu lake kabisaa hawezi likimbia. kama yeye hakusanyi Kodi kawe alikuja siku ile kwa mkutano alone kwa nini? kwanini asije na watumishi wa serikali wanaokusanya kodi? ni kwamba anajua hili ni jukumu lake yeye kwetu sisi.
 
Mdee achambue ushauri huu,asidharau na kuutupilia mbali.
Ndio maana tunasema wanasiasa wasitoe ahadi hewa,kama Chalinze nasikia Riz moko kaahi trekta kila kijiji na akishinda atakuwa na hardly mwaka mmoja tuu
Yani huu ni ushauri wa bure, Na kwa kifupi wala simsingizi yeye mwenyewe akiambiwa hili atakumbuka kama ubongo wake upo OK ila kama ni wa kuku hawezi likumbuka hili. Ni aibu sana, that day alijishaua sana akajifanya anawapigia simu wamiliki wa malori yanayo haribu barabara hii, huku akipiga SAVANAH yake baridiii as if tupo kwenye kikao cha kitchen party.
 
Hata kama hakusanyi Kodi Kawe ila yeye ndio Sauti yetu kwa Serikali. Sasa kama haongei habari zetu kwa serikali anaongea habari za nani? hili ni jukumu lake kabisaa hawezi likimbia. kama yeye hakusanyi Kodi kawe alikuja siku ile kwa mkutano alone kwa nini? kwanini asije na watumishi wa serikali wanaokusanya kodi? ni kwamba anajua hili ni jukumu lake yeye kwetu sisi.
Anaetakiwa kujua mambo ya kauchochoro ka mtaani kwenu ni Mbunge au Diwani?

That is No brainer.
 
Mdee achambue ushauri huu,asidharau na kuutupilia mbali.
Ndio maana tunasema wanasiasa wasitoe ahadi hewa,kama Chalinze nasikia Riz moko kaahi trekta kila kijiji na akishinda atakuwa na hardly mwaka mmoja tuu

Una funza kwenye ubongo, mdee anakusanya kodi yako?
 
Back
Top Bottom