Halima Mdee na wenzako mkataeni shetani na tubuni mrudi kule mnakopendeka

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
842
2,467
Kujikwaa na kuanguka sio mwisho wa safari. Kama binadamu mwaweza kuwa mlihadaika na kupotoka, lakini mmepewa muda wa kuomba radhi na kurudisha heshima yenu, fanyeni hivyo.

Kwanza mmegundua kwa nini sakata lenu limekuwa na moto mkali namna hii? Ni kwa sababu Halima na wenzako mlikuwa kipenzi sana kwa wana CHADEMA nchi nzima. Kwao ni sawa na MTU amfumanie Mke wake kipenzi aliyeishi naye miaka 20.

Mbaya ni kama Mke huyo badala ya kuangukia na kutubu kosa asamehewe yeye akakaza shingo kupambana kwa jeuri.

Halima na wenzako hebu angalieni mtapoteza marafiki zenu wangapi? Hivi kweli mupoteze Wanawake makini kama Maria Sarungi, Fatma Karume, Ananiel Nkya, Kijo Bisimba, Anastazia Shule n.k ili kujenga urafiki mpya na Jenister Mhagama, Shilole, Zuchu n.k kuimba mapambio ya kusifu na kutukuza?

Mna siku 30 za kujipanga na kuomba radhi ili kurudisha heshima yenu msipoteze muda huo.

Machozi, jasho na damu ndivyo vimejenga heshima yenu msikubali ipotezwe kwa peremende
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom