tunduruboy
JF-Expert Member
- Mar 16, 2013
- 423
- 218
• Asema hakuitendea nchi haki kwenye mikataba
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA)amemlipua Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Andrew Chenge, akisema kuwa alishiriki kwenye mikataba ya madini, lakini hakuitendea haki nchi yake.
Halima alitoa madai hayo jana mjini hapakatika semina kwa wabunge kuhusu rasimu ya sera ya gesi asili iliyoandaliwa naWizara ya Nishati na Madini na kufanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbali na Mdee pia baadhi ya wabunge nao walizungumza wazi kuwa viongozi walioishauri nchi kuingia katika mikataba yakifisadi ndiyo hao hao wanaisukuma ifanye haraka kuingia tena kwenye mikatabaya gesi asili hata kabla ya kuwepo kwa sera, sheria na kanuni.
Mdeealisema kuwa serikali imepuuza vurugu za kugombea rasilimali hiyo zilizotokea Mtwara na Lindi, na hivyo akataka umakini uwepo kwenye sera na sheria mpya yagesi ili nchi isirudi kwenye mikataba mibovu kama ile ya madini ya migodi yaGeita, Bulyankhulu na mingine.
"Mheshimiwa Chenge alishiriki kuishauriserikali kwenye mikataba ya madini, lakini hakuitendea haki nchi yetu," alisemaMdee.
Hojaya Mdee ilikolezwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy (CCM) ambaye lichaya kutomtaja Chenge kwa jina, lakini alionekana kumlenga yeye kwani wakati huondiye alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
Alisema wataalamu walioiingiza nchi kwenye mikataba mibovu wakatwe vichwa na kuitaja baadhi ya mikataba hiyo kuwa ni ileya ununuzi wa rada na ubinafsishaji wa Shirika la Ndege la Taifa (ATC).
Chenge ambaye kwa sasa ni Mbunge wa BariadiMagharibi naye alipata nafasi ya kuchangia katika rasimu hiyo ambapo alisemakuwa wabunge wanaweza kukataa nchi isichimbe gesi kwa kumsingizia hayatiMwalimu Julius Nyerere aliyetaka wapatikane wataalamu wetu kwanza.
Alisema watu wamekuwa wakimsingizia Nyerere kuwa alizuia rasilimali zisichimbwe na kufafanua kuwa wabunge wapende au wasipende lazima nchi iingie kwenye mikataba hiyo haraka.
"Watanzania tusiogope, sisi ndio viongozi wasasa. Tuangalie penye kasoro na tusahihishe. Lakini napenda kuwahakikishia kuwahatujawahi kufanya mambo gizani," alisema.
Kauli yake ilionekana kupingwa na baadhi yawabunge ambapo Mbunge wa Dole, Slyvester Mabumba alipoinuka kuchangia alianzakuomba radhi kuwa asieleweke vibaya kwa atakachokisema.
"Walioiingiza nchi kwenye mikataba mibovu yaRichmond na IPTL yawezekana wamo humu ndani, hivyo kamawizara wanakiri kuwa bado hatuna wataalamu wa kutosha tunaharakia nini?"alisema na kuhoji.
Madgalena Sakaya wa Viti Maaalumu (CUF)alipingana na kauli ya Chenge ya kuitaka Tanzania ifanye haraka kuingiamikataba ya utafutaji na uchimbaji gesi asilia akisema kuwa wananchi wameishaumwa na nyoka.
Alisema kuwa sera na sheria ya gesi asilialazima iseme kuhusu utunzaji wa mazingira kwani ile ya mafuta ilikuwa kimya nahivyo kuwapa mwanya wawekezaji kuharibu mazingira watakavyo.
"Serikali hii siyo ya kwanza wala ya mwisho,sasa kutaka kila kitu kifanyiwe kazi leo inaonesha kuwa hakuna nia njema. Vikovizazi vitakuja na ujuzi mwingine, haraka hii ya nini ya kutaka kumaliza kilakitu," alisema.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje aliungamkono kauli ya Mdee akisema kuwa lazima kuwe na uwazi kwenye mikataba ya gesiitakayosainiwa ili kuepuka kujirudia kwa makosa yale yale.
"Mwizi aliyekuibia jana, leo hawezi kuwamshauri wa ulinzi wa nyumba yako. Wale walioishauri serikali kuingia kwenyemikataba mibovu ndio hao wanashauri tena tuingine kwenye mikataba ya gesiharaka," alisema.
Wabunge wengine waliopata fursa ya kuchangianao waliunga mkono wenzao wakisema kuwa rasilimali zinazopatikana eneo lolote nchini ni za Watanzania wote na hivyo kupendekeza wananchi wapewe elimu yakutosha pamoja kuwekewa mazingira ya kunufaika na uwekezaji.
Walipendekeza kuwa sera inapaswa kuwawezesha Watanzania kuwa na hisa kwenge gesi hiyo, lakini wakataka ioneshe muda maalumuwa kukamamilika wa sera, sheria na kanuni.
Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangala (CCM)alitaka sera, sheria na kanuni za gasi asilia viwepo kwanza ndipo mikatabaifungwe ili kuepusha migogoro.
Mapema akifungua semina hiyo, Waziri waNishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa wale wanaopotosha kuwa wizara imegawa vitalu wana ajenda yaoya siri ya kuikwamisha nchi kiuchumi.
Alifafanua kuwa kilichofanyika ni kutangazavitalu hivyo ili wawekezaji waombe na kwamba Oktoba 25 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete atafungua rasmi mpango huo wa kujitangaza.
"Mei9, 2014 tunafungua hizo tenda kwa wale waliochukua nyaraka zetu na kesho yaketarehe 10 ndipo tunaanza kuvigawa hivyo vitalu. Wakati huo sera na sheria mpyaya gesi itakuwa imeshapitishwa na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili," alisema.
Alisema kuwa uchumi ni umeme na kwamba hakunanjia ya mkato, lazima kuzalisha umeme wa gesi wapende ama wasipende.
Tanzaniadaima