Ndugu zangu,
Mpashaji habari wangu amenijuza juu ya yale aliyoyaona Zenj; na hapa ni sehemu ya taarifa yake:
"Utafiti unaonyesha kuwa suala hili lilipangwa ******* na baada ya ***** jioni wakatoka watu takriban 60 hivi wakiwa na mapanga,visu,marungu,mashoka na kila mtu na chupa ya petrol na kwenda kuchoma vibanda hivyo hawakuwaruhusu kuchukuwa chochote.Kwa hiyo walichoma kwa ajili ya suala la ***** na ubara ambapo inasemekana wabara wamekuja kuchukuwa nafasi zao za kazi kwa kuwa wameajiriwa wengi kwenye mahotel.Kwa hiyo kitendo kimefanywa kwa sababu ya ***** ,utanzania bara na masuala ya kazi.Lakini kwa sasa wanaficha wanasema ni suala la ulevi na ukahaba.Tunajiuliza uvutaji unga si ulevi au ni bia tuu? Kama ni umalaya, je hawa vijana wa kiume wanaojiuza huku wanatoka bara?
Baada ya kuona hali ya huduma za kijamii za watu wale si nzuri niliongea na (***** kiongozi wa kundi moja la jamii) akanipa mablaketi na mashuka,vyakula ,nguo na vyombo.Ila ameniasa nisiseme zimetolewa na **** . Jioni ya jana tutawapelekea misaada na tumefanikiwa kupata waandishi wa cahannel ten,TBC na TVZ ili kuhamasisha watu wengine kuwasaidia.Hizo ndio some updates."
Naomba nirudie hapa kuwa hali eyote ya uvunjifu wa haki za binadamu ni tendo la kukemewa na kupingwa kwa nguvu zote kubalifu. walichofanya ndugu zetu Zenj kinahitaji kutolewa maelezo na kukoma, haraka.