falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,186
- 9,288
Saa saba na nusu usiku huu nilipokua natoka masaki naenda sinza kupitia kinondoni nimekutana na tukio la kuhuzunisha sana,
Nilipoanza kushuka bonde la mkwajuni kuelekea moroco hotel takribani njia nzima nilikua peke yangu naendesha gari ndipo kwa mbaali nikaona vijana watatu wanakimbia kuelekea moroco hotel huku mmoja kati yao akiwa yuko mbele na begi mgongoni huku wawili wakiwa nyuma wanamkimbiza
Nilipofika karibu niligundua wale vibaka walikua wanataka kumkaba yule wa mbele huku wakiwa na vitu mfano nondo zenye ncha kali,basi nikakimbiza gari hadi kuwa usawa sawa na yule wa mbele ndipo nilimsikia vizuri akiomba msaada huku bado wale vijana wakiendelea kuja,nilipofanya maamuzi ya kujaribu kusimama ili kumpa lift yule anaekimbizwa gafla nikaona vijana wengine wanne wanatokea kwenye bonde hilohilo la mkwajuni wakikimbilia gari yangu ndipo nilipoamua kukimbiza gari haraka huku nikimuacha yule jamaa amezingirwa.
Sasa kilichopolekea hadi kuandika uzi huu nimesikitishwa sana nilipofika kituo cha polis magomeni ili kutoa taarifa haraka nikakuta kumezungushiwa utepe unaonikataza kuingia kituoni hadi kesho asubuhi, basi sikuwa na la kufanya zaidi ya kuondoka huku nikiwa nimesikitika nikimfikiria yule mshkaji.
Sasa hapa nauliza jeshi la polis la tanzania lipo kwaajili ya kumlinda nani jamani mbona sielewi?