Hali ya ufisadi kwenye nchi yetu inasikitisha

Hali ya ufisadi kwenye nchi yetu inasikitisha

passioner255

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2019
Posts
6,803
Reaction score
13,034
Naomba watanzania tuamke Hali ya ufisadi ni mbaya Sana kwenye nchi yetu Chini ya huu utawala, tukemee huu ufisadi aisee.

Mfano kwenye utawala huu walisaini ujenzi wa Reli lot 3 na 4 ambao umesababisha hasara kubwa watu wamepiga pesa, kutokana na CAG lot 1, 2 na 5 uliosainiwa na Magufuli hamna shida yoyote lakini lot 2 na 3 watu wamepiga pesa.

Pia kuna upotevu wa B500 watu wameongea Pesa hizo kwenye miradi, ila kwakuwa watanzania hamjali Acha wajanja wapige pesa, huu utawala unanuka ufisadi natamani huyu Rais aondoke tu.

images%20(6).jpg
 
Kwani ni ufisadi au waliruhusiwa na mwenye nchi kula kwa urefu wa kamba? Kwani umemsikia Zitto Kabwe na genge lake wakiongea lolotekuulaumu utawala wa bi mkubwa baada ya ripoti ya CAG?
 
Kwani umemsikia Zitto Kabwe na genge lake wakiongea lolotekuulaumu utawala wa bi mkubwa baada ya ripoti ya CAG?
Vyama vya upinzani vimeona watanzania wengi hawajitambui, sasa kwanini umpiganie mtu asiye jitambua..?

Yani mtu mmoja asimame kutetea mamilioni ya watu lakini siku yeye akikamatwa kwa kuonewa wote wanao tetewa wanakunja mikia yao na kujidai wanamuachia mungu.

Ni upimbi wa kiwango cha lami! Hata mimi ningekuwa mwanasiasa ningekausha tu...

Yani watanzania tusipo amka na kujipigania wenyewe basi tuhesabu maumivu, kundi la wahuni wachache wataendelea kujimilikisha kila kilichopo juu ya hii ardhi ya Tanzania.
 
Naomba watanzania tuamke Hali ya ufisadi ni mbaya Sana kwenye nchi yetu Chini ya huu utawala, tukemee huu ufisadi aisee.

Mfano kwenye utawala huu walisaini ujenzi wa Reli lot 3 na 4 ambao umesababisha hasara kubwa watu wamepiga pesa, kutokana na CAG lot 1, 2 na 5 uliosainiwa na Magufuli hamna shida yoyote lakini lot 2 na 3 watu wamepiga pesa.

Pia kuna upotevu wa B500 watu wameongea Pesa hizo kwenye miradi, ila kwakuwa watanzania hamjali Acha wajanja wapige pesa, huu utawala unanuka ufisadi natamani huyu Rais aondoke tu.

View attachment 2582659
Tafuta nakala ya kitabu Cha am the state. Watu wapo bizeee kupambana na Marehemu muzilankende muyango 😂😂
 
Unashangaa nini mkuu? Kwani ulitegemea muujiza upi kwenye issue ya uadilifu? Tatizo mnaamini watu haraka na kuwaimbia mapambio mengi ya kuwasifu….!
 
Alafu tunasema TAKUKURU wapambane na rushwa kwa peke yao hawataweza kamwe tutawalaumu milele dumu
 
Huko Duniani wenye akili wanapambana kutengeneza nchi zao, sisi tunashindana kuiba na kutengeneza vikundi vya kusifia watawala.
 
Shida ukiona Mwenzako kaiba kajenga ghorofa au kanunua gari la Milioni 70 na wewe unajisemea " ngoja nami niibe nijenge ghorofa au ninunue BMW X6"

WAZALENDO NAMBA MOJA NCHI HII NDIO WANA MAISHA MAGUMU HAKUNA MFANO. NAO NI WALIMU.
 
Back
Top Bottom