Hali ya uchumi ni mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya uchumi ni mbaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dkn, Feb 3, 2012.

 1. d

  dkn Senior Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hali ya uchumi ni mbaya zaidi na viongozi wetu wamekuwa wakitupa data zisozo na ukweli hata kidogo kuwa uchumi unakuwa vizuri. Tumeona serikali ikishindwa kukabiliana na mambo mengi ambayo yameleta matatizo, mfano mgomo wa madaktari, walimu, halmashauri kutoweza kukamilisha au kuanza miradi iliyopangwa.

  Madaktari na walimu kama wafanyakazi wa serikali kuongezwa mishahara itakuwa vigumu sana kwa hali hii ya uchumi. Nani wa kulaumiwa na hali hii? Wananchi tulitegemea maisha bora bali hali imezidi kuwa mbaya na bado serikali inasema itatimiza ilani yake ya uchaguzi ikiwamo maisha bora kwa kila mtanzania.

  Tumeona maamuzi mabaya yakifanyika kuanzia Richmond, Rada, Kiwira, Madini n.k. na serikali imepoteza fedha nyingi na bado imeijingiza kwenye kesi za Richmond/Tanesco. Makusanyo ya ndani ni mazuri kama tunavyoambiwa TRA inategemea kufikia lengo lakini fedha nyingi zinapotea bila sababu ya msingi, matumizi mabaya ya fedha mengine yasiyo na tija kabisa, mfano kama Rais anakuwa na safari nyingi zinazotumia fedha nyingi za serikali na nyingi hazina manufaa kwa taifa.

  Tunazidi kukopa na tunakubali kabisa kusema, safari ya kuwaona wahisani nje ya nchi zinailetea serikali hela wakati kabisa tunajua madeni haya yatakuja kulipwa kwa njia ambazo zitatumaliza kwa kuingia mikataba hovyo na nchi wahisani. Imebaki tu watanzania waambiwe fanyeni kazi kwa bidii kujikimu na hali mbaya ya uchumi, je wananchi tuna imani gani na serikali kama uchapaji kazi wetu na ulipaji kodi utaliwa na watu wachache na hawafanyiwi chochote.

  Tungependa kuona serikali katika hali hii mbaya ya uchumi inafanya maamuzi magumu bila kujali, watumishi wote wa serikali walioiba fedha za serikali na wenye accounts nje ya nchi ambazo haziendani kabisa na kipato chake na wale wenye mali hapa nchini zisizoendana na vipato vyao mali zao zinataifishwa mara moja hata kama ni kuface consequence za kisheria baadaye ni sawa ila tutakuwa tumelinusuru taifa na kuleta imani kwa wananchi. Hatuwezi kuona wagonjwa wanakufa, watoto wetu hawapati elimu bora, sera mbovu za kilimo n.k. huku wato wanalindana, China wananchi wanafanya kazi kwa bidii na serikali yao haina mchezo kwa watu wanaocheza na mali ya umma.
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  sisi ofcn kwetu tuliishasahau kuwa kuna stahili za mfanyakazi. tumeambiwa tuishi kwa matumaini!
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Vielelezo vya kitakwimu kuthibitisha kwamba hali ya uchumi ni mbaya vingei-support thread yako. Aidha hawa unaotaka akaunti zao zitaifishwe mara moja ungewataja manake inaonekana unawajua kabisa. Isije ikaonekana kama ni majungu tu.
  Lakini pia tutambue kuwa tatizo ya kuyumba kwa uchumi ni la kidunia si la tanzania tu, mfano ni machafuko yaliotokea Misri, Libya, Tunisia na kwingine duniani ni matokeo ya kuyumba kwa uchumi katika mataifa hayo na ndiyo maana mpaka leo matatizo katika mataifa hayo hayajaisha pamoja na kubadilishwa kwa mifumo ya uongozi, jambo ambalo wananchi kwa kushinikizwa na watu wachache (Wanasiasa) walifikiri kuingia katika vita ingekuwa suluhisho. Tujikite katika kufanya kazi na zaidi kumuomba Mungu afungue milango yote itakayowezesha maisha yetu sote kuwa mazuri, tuiunge mkono serikali katika juhudi zake za kutatua kero mbalimbli badala ya kukimbilia kutoa mahitimisho ambayo mwisho wake ni kuingia katika matizo kama machafuko n.k
   
Loading...