Kambaresharubu
JF-Expert Member
- Jan 5, 2014
- 335
- 449
Katika moja ya sehemu muhimu ya kiuchumi kwenye manispaa ya Temeke ukiondoa Bandari ni eneo hili la viwanda la Chang'ombe - Mbozi Road, lkn kitu cha kusikitisha kuna kipande korofi junction ya Mbozi road/Manyara ambacho manispaa mwanzoni mwaka jana walifanya marekebisho ya drainage system lkn baada ya kuchimbua ile lami walishindilia vifusi tu...mwaka sasa unakatika toka wakamilishe zoezi, kibaya zaidi ule udongo umechimbika na kutengeneza mahandaki na kutokana na mvua hizi yale mahandaki yamegeuka kuwa madimbwi makubwa km ya kufugia samaki na kusababisha kero kubwa na uharibifu wa magari.
Nikikatiza tena baadae maeneo yale nitaambatanisha picha.
Nikikatiza tena baadae maeneo yale nitaambatanisha picha.