Shamba la Kulima mahindi kukodi Ekari 1 ni Tshs.40,000/= elfu 40. Kuhusu Kilimo cha Mpunga kwa sasa UMAFIA umeanza kuingia kwa kasi sana baada ya WACOMORO na WANYARWANDA kuvamia mashambani. Wacomoro wanakupa pesa tangu maandalizi mwishowe uwauzie Mpunga.
Mashamba yanamilikiwa na tycoon wenyeji kibabe tuu ukivuna mnagawana magunia ya Mpunga.
Wale waliowahi Mapema kununua hizi Mbuga za Mpunga kwa sasa anaweza tokea mtu mmoja akaanzisha kesi kwamba hilo shamba ni lake. Kwa kifupi umafia umekuwa mwingi sana. Unaweza kulima Mpunga mavuno akaja kuvuna mtu mwingine tena akiwa na SMG zimesimamia zoezi. Kwa kifupi Kilimo cha Mpanda na Sumbawanga bado hakina formula ingawa mavuno yapo mengi