Hali ya Fedha mfukoni ni mbaya kwelikweli, Kwenu vipi waungwana?

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Jamani siasa ni maisha, Ebu tuelezane wajasiria mali wenzangu.

Hii hali ya mfukoni mnaionaje? Mbona mifuko ya watu nahisi imetoboka sana. Namaanisha mfukoni hela wengi hawana. Nina ka biashara kangu sehemu flani ki ukweli pato limeshuka mpaka naingia uoga.

Tatizo nini haswa? Kila ninayemuuliza analia kama mimi. Baadhi wanasema nisubiri Bunge la bajeti lipitishe 2016/2017 najiuliza upo uhusiano kweli?

Hali ikiendelea hivi, Pango linaweza kuwa mtihani achia mbali watoto shule na mahitaji yao muhimu.

Naomba Mungu na kule Zanzibar patokee maridhiano maana wafadhili nao wakifunga koki ndio balaa zaidi.

Mungu atusaidie wakuu hali ni ngumu kweli kweli sijuwi tu kwenu.
 
Ukweli hali ngumu, mpaka nimebadili life style, nimepanda bustani ya mbogamboga, maji ya kunywa nachemsha. Yaani hapa nikinunua kiroba cha mchele, juzi kati nilikuwa mkoani nikanunua mahindi, nimeyasaga Kuwa unga wa dona.

Mambo yanakwenda halafu Nina kuku wa kienyeji nafuga. Hapa mwendo wa kubana bajeti.
 
Hiii hali mimi naiita tuheshimiane.

Kwa mwendo huu naona wengi wetu tutageuka kuwa wakulima iwapo serekali hii itaweka mazingira mazuri kwa mkulima kama kushusha pembejeo na kuonda kodi za manyanyaso.

Wale watu waliozoe kwenda mjini kufanya deal za katika yaani madalali kazi wanayo. Mimi miaka michache iliyopita nilinunua shamba kabuku nikawa naliendeleza kidogokidogo. Sasa wangalau vijana wa shambani kila wiki wananitumia hela ya mauzo ya mbogamboga na mauzo ya mayai. Ila kama ni mtu ulikuwa unangoja kutengeza risiti fake ofisini imekula kwako.

Na huu ni mwanzo tu, mpaka mwisho wa mwaka huu wale wanaoishi kwa ujanja ujanja ndio mwisho wao ni lazima sasa wakatafute kazi za halali na hakuna zaidi ya kilimo kwani ajira hakuna.
 
wewe nilivyokuwa nakwambia kuwa ni kibaka hapo mjini na hisitoshe hauna hata account na kama ubavyo hina buku 17 tu.usiseme watu hawana pesa sema mimi sina pesa.na bado


swissme
 
safi sana...sasa watu waheshimiane mtaani...mtindo wa kujenga maghorofa non stop tangu mwanzo mwisho uishe..alafu unakuta Karani tu wa TPA au TRA Anamiliki maghorofa kibao
 
Ukweli hali ngumu, mpaka nimebadili life style, nimepanda bustani ya mbogamboga, maji ya kunywa nachemsha, yaani hapa nikinunua kiroba cha mchele, juzi kati nilikuwa mkoani nikanunua mahindi, nimeyasaga Kuwa unga wa dona. Mambo yanakwenda halafu Nina kuku wa kienyeji nafuga. Hapa mwendo wa kubana bageti.
Hongera ulipata hata kasafari, vimeingia vichenji kidogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom