Hali ya elimu katika jimbo la Iramba Magharibi

Imebidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Posts
339
Reaction score
163
Moderator, najua hii mada inaangukia jukwa la elimu, lakini naomba msihamishe hii, angalia kwa muda wa siku chache.

Juzi nimemsikia Mwigulu Nchemba akitamba sana kuhusu maendeleo ya elimu nchini na hasa kwenye Jimbo lake. Hii ni pale alipohojiwa na VoA.

Sasa Tarehe 01 Septemba 2013 Dk Kitila Mkumbo alialikwa na umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotoka Iramba kushiriki mjadala wa namna ya kuboresha elimu Iramba na alipewa nafasi ya kuwa mgeni rasmi. Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine alieleza hali ya elimu katika Jimbo hilo na akatoa mapendekezo yake ya namna ya kutoka hapo. Alionyesha kwamba hali ni mbaya sana. Nawaletea dondoo za yale yaliyokuwemo kwenye hotuba yake ambaye aliigawa kwa wajumbe. Of course hotuba yake ilileta kasheshe na manusura Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Lulumba afukuzwe na afisa elimu sekondari kwa kumkaribisha Dk Mkumbo kwa maelekezo ya mkuu wa Jimbo, Mwigulu. Bahati nzuri hotuba yake aliigawa kwa Afisa Elimu na watumishi wa halmashauri ya wilaya na watu waliifurahia. Mwigulu alikasirika sana kwa nini yeye hakupewa nafasi ya kuwa mgeni rasmi. Anyway, hii hapa ndiyo hali halisi ya elimu huko Iramba.
____________________________________________________________________________________________
· Jumla ya Wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2012: 1804
o Waliofaulu: 376, sawa na asilimia 20.8
o Jumla ya waliofeli na waliofaulu kwa ngazi ya Daraja la Nne: 1393, sawa na asilimia 77.2
o Waliofaulu somo la hesabu: 83, sawa na asilimia 4.6.
o Kati ya shule tano zilizofanya vibaya zaidi kimkoa (Singida), tatu zipo katika Wilaya ya Iramba (Jimbo la Iramba Magharibi) ambazo ni: Mgongo 94/94, Kyengege 91/94 na New Kiomboi 92/94. Kyengege ndiyo Kata anayotoka mbunge wa Iramba Magharibi.
o Shule ya mwisho kimkoa ipo katika Wilaya ya Iramba (Jimbo la Iramba Magharibi), nayo ni Shule ya Sekondari Mgongo.
Kwa matokeo haya ni vijana 35 pekee wenye uwezekano wa kujinga na kidato cha tano mwaka 2013 kutoka Wilaya ya Iramba, na ni hawa pekee wenye uwezekano wa kujiunga na Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu mwaka 2015.

Sasa hiyo elimu bora ambayo Mwigulu alikuwa anatamba nayo huko VoA ni ipi?
 
Hapa umemumaliza mtani wangu , ila nakushauri uombe mafundi wakutengenezee protector ya chuma ya kufunika mwili mzima , ama sivyo hatari unayo.
 
mwigulu yupo majuu anakula bata, akisharudi atakuja kuboresha hiyo elimu wanaIRAMBA
 
IRAMBA magharibi wamlilia mbunge wao Mwigulu Mnchemba.

Wanasema ukistaajabu ya Mussa utaona ya Mwigulu,
Wakati mbunge wa Singida magharibi Mhe. Mwigulu Mnchemba anapasua masafa ya nchi wapiga kura wake wanamlilia kweli aende akawasikilize matatizo yao kwani shida zimewakaba hadi shingoni. Wanamstaajabu mbunge wao ambae wakati rais wake anachanja mbuga duniani yeye mbunge anachanja mbuga inchini akiwawakilisha wanainchi ambao hawakumchagua akiwaacha wao katikati ya lindi la matatizo. Nimepita jimboni mwa huyo mbunge wapiga kura wake wakanieleza yafuatayo kwa mdomo wao:-
Shida zinazowakabili-

1. Njaa kali.

Wana uhaba mkubwa wa chakula mvua zilikuwa haba sana ukitilia maanani wenywe wako kwenye bonde la ufa inabidi kupata mvua za kutosha ili wavune mtama (lugugu) wacha mahindi, kwa hiyo wanauhaba mkubwa wa chakula familia nyingi karibu % 90 katika jimbo la Mwigulu wanakula mlo mmoja na huo mlo mmoja hawashibi. Watoto wa shule wanashindwa kwenda shule shauri ya njaa, pia wakirudi nyumbani saa 6 wanalala inje ya nyumba shauri ya njaa kali ndani hamna kitu na wazazi wao hawapo wamekwenda kutafuta vibarua, wengine wanazirahi.
2. Umasikini wa kipato.
Wanaumaskini mkubwa wa kipato wachilia mbali njaa inayowakabili, hawana zao lolote la maana la biashara,ajira wanayoitegemea ingalao kupata kipato ili kutatua matatizo yao ni ombaomba kwenye treni, na biashara za ovyoovyo kwenye treni yakati biashara kama kuuza ujugu, vikapo , vindege, vifilimbi vya miti, ukwaju na ubuyu, ni vibiashara vya kijinga jinga tu, vijana wengi wamekimbia jimbo wasichana kwa wavulana wameenda kutafuta ajira mjini na wengine wameenda kutafuta vibarua vya kulima tumbaku katika vijiji kata ya Igwisi urambo.

3. Ukame mkali.

Kuna ukame wa hali ya juu, ukame unawakabili watu na mifugo, mifugo kuanzia vijiji vya Kintinku, Igose, Makutupora Kirimatinde Salanda, Ulyampiti, Msigili hadi Sherui mifugo wanakunywa mgwao, yaani wanakunywa leo siku inayofuata hawanywi maji.Maji yenyewe wanayapata kwa kuesea kwa kutumia Nkosi,wanadamka usiku kwenda kwenye visima walivyochimba wenyewe ili kuchotelea maji kwa kutumia nkosi na kujaza mrambo ili mchana mifugo waje wanywe, kazi hiyo ni ngumu sana inawafanya vijana wengi kukimbia makazi yao au kuwa ni ajira kwa wenye uwezo, mtu unafanya kazi hiyo ngumu halafu anaishia kupewa chakula tu jioni.

4. Wizi wa mifugo.

Kuna wizi wa mifugo wa hali ya juu, hii ni kutokana na njaa kali, mifugo inaibiwa nyumbani usiku au mchungaji ananyang`anywa mchana kweupe machungani, mifugo inaibiwa kiasi kuna tishio la mifugo kwisha kwa wizi, wengine huiba mbuzi na kwenda kuchinja polini na kuishia kula nyama shauri ya njaa.

5. Magonjwa:

Tunakabiliwa na magonjwa ya kuambikiza, magonjwa yanayotusumbua ni Malaria na kichocho, malaria inatusumbua kwa ajili ya joto hapa jimboni kwa Mwigulu ni bonde la ufa yaani ardhi imetitia chini hivyo joto kweli usiku na mbu ni wengi , kwenye vituo vya kutolea pia uwezo wa kukata bima ya afya hatuna kwa sababu ya umasikini wa kipato, Kichocho kinasumbua sana hasa wanafunzi ,shule kama Ndago karibu wanafunzi wote wana kichocho dawa ya Parazenguantel hamana katika vituo vyote hadi hospitali ya mkoa ya Singida, halafu dawa yenyewe ni ghali. Pia jimbo la Iramba magharibi karibu lote linakabiliwa na tatizo la mishoo kwa ajili ya kula nyama mbichi za wizi.

6.Mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na secondary
Mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na secondary zimekidhili jimbo la Iramba magharibi katika majimbo yote ya singida Ilamba magharibi ndio inayoongoza kwa mimba za utotoni na kwa wanafunzi mashuleni, wanaowapa mimba wanawapa rushwa wazazi wao halafu hawawapeleki panapohusika ili sheria ichukue mkondo wake yeye Mwigulu mguu na njia hayaangilii haya jimboni kwake kazi kuitangaza CHADEMA tu.

Ushauri kwa Mbunge wa Mwigulu

Aje akae jimboni ili waweze kusaidiana kukabili matatizo haya , huko unakozurula kwani ndiko walio mchagua? Aache kuhangaika na LEMA kwani mbunge huyo hamwezi wanaweza wenyewe waliomchagua. Kupenda ni sehemu ya uhai , kumeambatana na uhai kupenda hakuwezi kwisha mpaka uhai umetoweka kwa hiyo kama Arusha wanampenda mbunge wao Mwigulu hata ufanyeje unajisumbua tu njoo jimboni utusaidie wapiga kura wako tunakwisha. Huyo LEMA unayempiga vita yeye anawapigania wapiga kura wake hadi saa ingine bungeni haendi hadi anafungwa jela mahabusu wewe Mwigulu unazurula tu unatusahau,

Kama mbunge una uwezo kutusaidia kupata dawa hasa za kichocho, kulobe chakula kije jimboni ingalao tutanua, Kwenye jimbo la Tundu Lisu mashuleni wanafunzi wanapata mlo wa mchana kupitia Pragram ya WFP, Mbunge wetu Mwigulu yuko wapi na sisi tupate mpango huu. Njoo tusaidiane kuandaa mkakati wa kukabiliana na wizi wa mifugo, njoo tujipange tuweze kukata bima za afya kwa watendaji wa kata ingalao zituwezeshe kupata
matibabu hata hayo kiduchu.

Mbunge wetu Mwigulu njoo jimboni sisi wapiga kura wako tunakulilia kwani hiyo jeuri uliyopewa na Rais kwamba wewe unakabiliana na wapinzani hukimbilii polisi isikuvimbishe kichwa kiasi unasahau wajibu wako. Wacha kujishebedua na mkutano huko Dar. Njo site uone mwenywe serikali ya chama chako ilivyotufanya mbaya kwa kutufanya tuwe maskini wa kutupya, ile kambi ya wakoma ya sukamahela imeanza kujaa tena wengi wa wagonjwa wanatoka wilaya ya Iramba.

kichwa chako kama cha panzi mkuu mbunge na mambo ya ukame anahusika nayo vipi,kufeli kwa wanafunzi mbunge anaingiaje hapa kwa yeye anafundisha darasani au yeye ni ofisi ya elimu mko unaongea kana kwamba hujitambui vile au hujui useme nini.
 
kweli mkuu umevurugwa halafu kilaza balaa,ukame,wizi wa mifugo,mimba shuleni,magonjwa ya kuambukizwa hapa mbunge kaingiaje?.
 
Mbunge kwenye hayo mambo anaingia kwa sababu ndo jinsi huwa anajisifu kwamba constituency yake inmaendeleo,ambayo c ndo haya?
 
Mwigulu ni popompo

tatizo sisi wanyiramba tunapenda ubwete.Hiyo shule ya Mgongo watoto wanafundishwa na wenzao baada kupiga tuisheni mjini.wanaishi kwny vitembe hakuna umeme.nimechukua mkopo mwakani nitahakikisha wanapata hostel na umeme wa jua.Dr.Mkumbo jiandae kwny uzinduzi
 
Mi kila siku huwa najiuliza mwigulu alipenyaje hadi kuwa mbunge wetu iramba?? Yaani hata maccm menzake aliyashinda?? Na hao alowashinda sasa wakoje??

Hali halisi ya elimu jimbo la iramba magharibi ni mbaya kuliko maelezo. Sisi tunaokaa huko tunajua ila mwigulu analifanyia siasa ili aendelee kuwa mbunge.katika shule zote iramba ukipata alopata div 2 shukuru. Huwa najiuliza, matokeo gani hayo mwigulu anayojivunia iramba??

Uchmbuzi kama huu wa Dr. Kitila ingekuwa vema ukasambazwa iramba yote kwa mwenye macho na akili aone na atofautishe facts na siasa za mwigulu zenye nia ya kuididmiza iramba.
 
Ni kwaeli WANYIRAMBA ni watani wetu sisi wambulu ila Mwigulu Lameck Nchemba (mb) na Salome Daudi Mwambu (mb) [iramba magharibi na mashariki] hawana hadhi ya kuwa watani wetu kwani wananuka damu na si wanadamu wa kawaida kwani ni washirikina wa ajabu sana,nawasihi watani zangu wasirudie makosa 2015 kwani kuna vijan wengi wenye uwezo kitaaluma na wala hawtumii ushirikina kama hao wa sasa.
 
Back
Top Bottom