Hali ya Bobi Wine ni mbaya na familia yatishiwa na Serikali

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
-Jamaa wa familia yake walieleza kuwa hawajui anayewatumia vitisho hivyo

-Walisema kuwa hawatatishwa na vitisho vyenyewe na kuwa wataendelea kupigania uhuru wake

-Walikariri kuwa Bobi alihitaji matibabu na kuwa hali yake ya afya haikuwa nzuri

-Mkewe Bobi alisema kuwa mumewe alikuwa akiteswa kizuizini na nusura afariki kwa wakati mmoja

Jamaa wa familia ya mwanasiasa na msanii maarufu wa Uganda, Robert Kyangulanyi anayejulikana kama Bobi Wine wamedai kuwa wamepokea vitisho vya kifo tangu Bobi alipofungwa gerezani.

Tangu Bobi alipokamatwa, jamaa wa familia yake wamekuwa wakijaribu kutafuta uhuru wake huku mkewe akisema kuwa hali yake ya afya ilizorota sana

Jamaa hao wa Bobi walihofia maisha yao kutokana na vitisho vya mauaji dhidi yao wakisema kuwa hawajui anayewatumia vitisho hivyo.

Hata hivyo, walisema kuwa hawatatishwa na kuwa wataendelea kutafuta uhuru wa Bobi.

Jamaa wa familia ya Bobi Wine wamesema wanahofia maisha yao baada ya kupokea vitisho vya mauaji.
Mwanasiasa huyo mwenye ushawishi wa upinzani alishtakiwa kwa makosa ya uhaini na anazuiliwa katika kambi za kijeshi.

Alikamatwa pamoja na wabunge watatu na waandamanaji wengine baada ya uchaguzi mdogo mjini Arua, Kaskazini mwa Uganda kugeuka kuwa ghasia.

Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki alishtakiwa kwa kuurushia jiwe msafara wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni na shtaka la kuwa na bunduki.

Mkewe Bobi, Barbie Kyangulanyi alieleza kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumamosi, Agosti 18 jinsi hali ya afya ya mumewe ilivyozorota na kuwa alihitaji huduma za matibabu kwa dharura.

Barbie alieleza kuwa Bobi hakuweza kusimama pekee yake na kuwa alikuwa na uso uliofura na kuharibika.

Ujumbe wa Marekani ulizungumzia kudhulumiwa kwa wabunge wanaozuiliwa na kusema kuwa walihitaji kuzuiliwa kwa utu.

Ujumbe huo ulimtaka Museveni kuionyesha dunia kuwa serikali yake ilifuata katiba.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Our Stone aka Jiwe is learning from the best. Cha ajabu mijitu kama Stone na wenzie wanaishi mpaka kuwa vikongwe, sijui kwanini muumba asiwachukue haraka kutuokoa na kadhia hizi za binadamu waliojitwika uungu mtu, kwa tamaa za matumbo yao kujimilikisha haki ya kuamua hatma ya maisha ya wenzao.
 
Back
Top Bottom