Hali si Shwari Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Hali si Shwari Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
Ripoti zinasema kuwa hali si shwari ndani ya Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa, licha ya sintofahamu kufuatia kusitishwa kwa zoezi la ugawaji wa vitambulisho katika baadhi ya maeneo, utendaji ndani ya taasisi hiyo hauko vizuri.

Madudu mengine ndani ya NIDA ikiwemo kupeana kazi kindugu (karibu watu wote wanaofanya kazi data centre, iliyopo jengo la BMTL, Victoria wameajiriwa bila utaratibu rasmi na wanajuana na wakubwa wa NIDA). Jambo lingine ni ndugu na vimada wa mabosi wa NIDA kutaka kupewa huduma za vitambulisho bila kufuata utaratibu rasmi kwenye vituo vya ugawaji vitambulisho, jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wafanyakazi hao.

Malipo ya wafanyakazi wanaoenda kufanya kazi za nje ya kituo huwa hayapo, au ni ya kuzungushwa, huku wakiambiwa na baadhi ya watu walio karibu na wakuu wa idara kuwa hela ipo, lakini wasipofuatilia wataambulia patupu.

Tuhuma zingine ni pamoja na mamlaka kutuhumiwa kuajiri watu ambao aidha hawana elimu stahiki ama ambao utendaji wao ni dhaifu kwa kuwa tu wana mahusiano ya kindugu/mapenzi na hao wanaoitwa vigogo wa taasisi hiyo (wakuu wa idara na mameneja).

Kinachotarajiwa: Kutokana na matatizo hayo ambayo ni ya muda mrefu na hayana dalili ya kutatuliwa kuna uwezekano wafanyakazi wa NIDA wakashusha utandaji wao kwa makusudi, hii ni kwa mujibu wa mtu aliye karibu.
 
NIDA kwa ujumla sijakubali utendaji kazi wao.
 
Vidole vya mafundi ujenzi havisomi hawa NIDA ni tatizo lingine kwenye Hii nchi kama ccm.
 
hamna jipya hapa, taasisi zote za serikali huu ndio mtindo, ajira za kujuana kindugu au kimapenzi obvious lazima zitaleta ufanisi duni!!! njia pekee ya kumalizana na uozo huu ni kuiondoa hii serikali madarakan na kuweka wengine kwa njia ya demokrasia au wakikataa basi kwa nguvu ya umma maana hamna namna!!!
 
Inavyoonekana nida kunachangamoto nyingi.
 
Kuanzishwa kwake kulikuwa na nia njema kabisa,watendaji wamekiharibu na sasa kinaelekea halijojo.Serikali iunde tume moja kwa moja kubaini ufisadi,kunusuru upatikanaji vitambulisho vya uraia
 
Kuanzishwa kwake kulikuwa na nia njema kabisa,watendaji wamekiharibu na sasa kinaelekea halijojo.Serikali iunde tume moja kwa moja kubaini ufisadi,kunusuru upatikanaji vitambulisho vya uraia
Jamani tumechoshwa na tume, kila kazi inayofanyika Tz, mwisho wa siku ni kuunda tume tu?!!, na hata hizo tume zinapoundwa nini hutokea? kama sio chaka la kuendelea kutiana hasara tu, kwani wao wanaoanzisha hiwa wanajua kabisa kuwa program hiyo haitafika mbali kutokana na maandalizi ya zima moto, na wadau huwa wanatoa angalizo lakini kwa kuwa wahusika wanakuwa wameshaweka cha juu, wahasikii na hata linapobuma cha kwao wameshachukua wana hasara gani? mfano hki BVR, nayo ibume mseme ni bahati mbaya?! mipango mingi ya serikali inakufa hata kabla haijaanza ndugu.
 
Ni kweli kabisa mtoa uzii. .... Wakati nimemaliza tu chuo..... Nilikuwa cheap labor wa kugawa fomu...... Takribani wale waluokuwa wanajiita wameajiriw nida ni form four failure.. Wana udugu na mabosi wa nida .....utendaji ni ziro kabisa.... Halafu wanamalingo sana....
 
Last edited by a moderator:
Mh ndio maana mwenyenyumba leo hajaenda kwa job
 
aiseee babayangu hawa jamaa kwele ni wapumba~~vu huwa wanawachukuwa wale vijana wa darasa la saba jkt hawana elemu yoyote wanawafanyisha kazi bila malipo yoyote
 
siku CAG atakapo kagua NIDA nadhani MD Maimu atafata nyao za kina Mramba pale kisutu, huyu mtu kapiga pesa ndefu sana nida kanunua nyumba mikocheni akazivunja na kujenga Club inayoitwa MRC.
 
Hivi kuna kitu tunaweza kuendesha kwa ufanisi kweli? Tumelaaniwa na nani?
 
siku CAG atakapo kagua NIDA nadhani MD Maimu atafata nyao za kina Mramba pale kisutu, huyu mtu kapiga pesa ndefu sana nida kanunua nyumba mikocheni akazivunja na kujenga Club inayoitwa MRC.
MRC, pale ambako TBC huwa wanafanyia kipindi chao cha Club Raha Leo? Huwa naona Yutong za NIDA zimepaki pale, tena usiku...
 
Back
Top Bottom