Huyu anaweza kwenda bungeni. Kwenye nchi hii hilo ni la kawaida.
Nakumbuka mwaka 2005, nikiwa Mza, mgombea wa CCM alikuwa akizindua kampeni zake. Wapambe wake walianza kwa kumtambulisha na baadae wakamkaribisha ajitambulishe na aongee na wananchi. Bwana huyu aliposimama, alijitambulisha jina lake na akaongeza kwamba, "Mimi ndiye mgombea ubunge katika jimbo la..." akainama kuwauliza wapambe wake na sauti ilisikika kwenye kipaza sauti "Jimbo la wapi......", wakamjibu "Nyamagana".... Huyu bwana alishinda na akaingia Bungeni na baadae akawa waziri wa wizara nyeti tu hapa nchini. Kwa hiyo sio ajabu huyo nae hata kama mnamuona kama amelzaimishwa, akashinda na kuingia bungeni.