Hali ni tete Tanzania

Hali ni tete Tanzania

Mnajua kujifariji mtandaoni. Halafu ikija 2020 mnaanza kupiga deki barabara na kuzungusha mikono, ha ha ha kazi mnayo.
 
Na nchi zilizoendelea walianza maendeleo ya vitu ndipo ikaja watu.Yaani walianza na miundombinu ambayo ndio ilipelekea watu kufanya shughul za kuwaletea maendeleo kuwa Rahisi. Hata Africa wakoloni walianza na miundombinu
Je, walianza pia na kuua watu na kuteka?
 
Na nchi zilizoendelea walianza maendeleo ya vitu ndipo ikaja watu.Yaani walianza na miundombinu ambayo ndio ilipelekea watu kufanya shughul za kuwaletea maendeleo kuwa Rahisi. Hata Africa wakoloni walianza na miundombinu
Ndo nn?? We muongo na hupati LIKE yangu wewe
 
Waafrika wameshindwa kujiongoza sio kujitawala. Hatuhitaji watawala, tunahitaji viongozi wanaojali maendeleo ya watu na sio vitu.
Hadi tubadili mfumo wa uongozi ndipo matatizo ya waafrica yatakwisha uliopo wa MTU mmoja kuongoza wengi atufiki nchi inatakiwa iongozwe na watu sio mtu. Maamuzi ya nchi yaongozwe na watu.Huu mfumo wa kitu kinautwa raisi kama ndie kiongozi tutasubiri sana Africa ni heri tuwaite wakoloni watuongoze kuliko hawa wakoloni weusi. Mfumo wa uraisi haufai Africa unafaa ulaya na marekani kwenye nchi zilizoendelea.Kiongozi yeyeto kiafrica inatakiwa aundiwe mfumo wa kumcontrol ili afanyike BARAKA na si laana, yanayoendelea Africa nzima yanasadiki maneno ya mwanazuoni mmoja mwaka 1946 kuwahi kusema,Mwafrica hana uwezo wa kumuongoza Mwafrica mwenzake zaidi atamtawala Kwa kumletea umasikini Mwafrica mwenzake kumua,kumtesa,kumteka,kumfilisi na madhila kila namna.Imepita miaka mingi maneno hayo yanaishi.Africa inahitaji ukombozi wa pili dhidi ya wakoloni weusi baada ya ule wa awali wa wakoloni weupe.
 
Akili kubwa wewe! Big up. Swali langu ni moja tu; je tunavukaje hapa ili tubaki salama?!
Kuna njia kama tatu ya kujikwamua kutoka katika hili balaa..
1)Serikali ikae meza moja na Wapinzani ili kuokoa taifa
2)Serikali kukubali matakwa ya nchi wafadhili
3)Bunge lijadili uwezo wa Rais wa kuliongoza Taifa
 
True wakauvaa mtego wa Mbowe kuruka dhamana wakamsukuma ndani baada ya kutoka ulaya,mabeberu wameona hawana hata cha kujitetea kila kitu live,wakaingia mkenge kuwateka kina Dada wale waliojifanya kuja kuchunguza hali ya Uhuru wa habari,sasa hawana cha kujitetea kujibu hizo Hoja 15 maana walishindwa kung'amua mitego ya kinadada wale wanaharakati na mtego wa Mbowe, Mbowe atakuwa ndani akiwacheka waliokuja mjini wakubwa walivovaa mtego wa kumuweka ndani
Aiseee naona kichaa jiwe akianza kujamba bila break!Yule mpambe anayesimama nyuma yake ana kazi nzito ya kuvumilia harufu kali.Na ninashauri wawe wanakagua pants zake baada ya hotuba..Safi sana.

Leo jamaa alikuwa mpole sana,na sitashangaa akianza kutoa hotuba kwa kusoma a perfectly edited speech, with a carefully chosen tone/language,badala ya "kupopoma" mihotuba isiyo na staha.Alikuwa anajinasibu yeye ni KICHAA,ngoja akutane na lWAPUMBAVU a.k.a Zombies zaidi yake.

Kuhusu Tundu A. Lissu:Bravo sana bro!Mungu akupe maisha marefu.Nilijua pale Brussels utakuwa pale strategically, na unacheza kete zako vyema kabisa.Walifikiri ukiwa nje ya Bunge la Dodoma utakuwa no longer a threat,au utaishia kuwa unashangaa magoli anayofunga Mbwana Samatta pale Genk...kumbe kule chalii wangu una Bunge lako mwenyewe (Bunge la mtu-mmoja),lililo na Impact kubwa internationally kuliko Akudo!..Watanyoooooka kama rula.

Wale wanakwaya Wasabato wa Rwanda waliimba kweli:MUDA WA KILIO UMEKWISHA..(Tulilia,sasa ni zamu yao kulia).
 
Martin Maranja Masese kaandika. Mchana wa siku moja, Rais wangu anasikika akisema tupo pazuri tusitetereke maana nae hatetereki na hayumbishwi maana ni. Kweli tunapaswa kujivunia kupata "Rais JIWE kweli kweli" anasema tusitishwe na mabeberu, tunaweza kuwakopesha hata sie!

Siku zinakwenda mbele, uso wake unabadilika, anaonekana ni mwenye mengi kifuani, macho yakiwa yanajieleza, anakwenda mbele ya vinasa sauti akiwa mwepesi, unamtazama usoni ni kama anaomba msaada kwa watazamaji, watu wanataka kusikia atasema nini le kiongozi wao!

Anaongea kwa tahadhari kubwa sana leo, anatueleza kwamba ni Rasmi nchi yetu ipo VITANI. Vita ya nani? Vita gani? Anatueleza VITA YA KIUCHUMI. tunashangaa, nae anatushangaa, anasema "Bado wananchi tumelala usingizi wa PONO, yaani FOFOFO"

Sasa tunajiuliza, kwani tukiacha kulala huo usingizi uliopewa jina la FOFOFO ndio tutaacha sasa kukopa pesa World Bank? Tutaacha kuwalilia waturuki watupe msaada wa kuijenga SGR? Hatutakwenda UCHINA!?

Mimi nilipoona tumefika hatua ya kuwaomba kwa kupiga magoti kwa RSA nikajisemea "kweli omotwe no oghomonto" yaani SAUZI tuliwapa UHURU sie, leo tunawaomba mkopo wa kujenga SGR? TUMEKWISHAA! TUPO PABAYA!

Yule mfalme wa Morocco akatuletea porojo za kutujengea uwanja. Mkubwa wa soka pale Dodoma, sijui kwa 'conditions' zipi, Rais wa Misri nae akasema anataka kutujengea kiwanda cha kuchinja nyama na kusindika. Hadi leo KAVU!

Wengine kwa sababu hatuna kumbukumhu dhaifu, tunarejea nyuma, tunamkumbusha mheshimiwa, tuliwahi kumuuliza Waziri wetu wa Fedha, UCHUMI gani ambao ameusomea? Anasem tupo pazuri, lakini Bajeti haitekelezeki hata nusu katika fedha za maendeleo,

Waziri wa fedha anasema nchi ipo pazuri, wakati huo benki zinafungwa biashara zinafungwa, Wafanyabiashara wanahamia nchi Jirani Ajira hakuna, huo uchumi gani ambao unakuwa kwa kasi? Uchumi unakuwa, wananchi wanalia hawana fedha maisha magumu?

Anakuja Gavana wa benki kuu, anasema "chungu vha Rais" kipo imara, yaani fedha za wa Tanzania Gavana anaziita "chungu cha Rais?" kweli hawa watu wametuona "poyoyo", anasema hayo hadharani, sio kwenye vikao vya ndani..

Gavana siku nyingine anakuja mbele yetu anasema kuna 'reserve' ya kutosha ya fedha za. Kigeni, kwamba. Zinaweza kuendesha nchi kwa. Muda wa miezi sita bila kuomba msaada kwa yoyote Gavana huyu anatueleza hayo hadharani, akirejea maneno ya "chungu Kipo imara"

Siku zinakwenda, leo Waziri yule wa fedha ambaye alitueleza kwamba uchumi wetu upo imara kwamba miradi mikubwa ya ndani tunaweza kutekeleza kwa fedha za. Ndani na sio mikopo, ingawa bado TUNAKOPESHEKA, leo anasema NCHI INAPITA KWENYE KIPINDI KIGUMU KIUCHUMI..

Sasa naelewa kwanini Rais wangu alionekana mwenye taswira ya kuomba msaada usoni akiwa ni mwenye "frasitresheni" na akiwaeleza wananchi, washirikiane nae katika maombi, kumuombea! haya yote yameletwa na mambo mawili kwa mtazamo wangu, nimebaini yafuatayo!

Wasaidizi waaminifu wa Rais, haswaa huyu Gavana na Waziri wake wa fedha, hawana weledi wa utendaji, wanamiliiki HOFU, hawamuelezi ukweli Rais, kuna sehemu watakuwa hawasemi ukweli, kuhusu HALI YA UCHUMI wa Tanzania.. (labda)

Pili, kutegemea mikopo na misaada kuendesha nchi, wahisani wamefunga baadhi ya misaada, wameondoka, kwa.l sababu ya kuwa TEGEMEZI, fedha hakuna, hivyo fedha za kuendesha miradi ni HAFIFU..

Maana Waziri leo anatueleza "kutokana na wahisani wengi kuacha kutoa misaada na mikopo yao nchi sasa INAPITA katika kipindi KIGUMU kuliko wakati wowote" Waziri yule ambaye alitueleza Bungeni kwamba nchi yetu ipo imara kiuchumi na haitegemei fedha za wahisani kujiendesha katika miradi yake..

Sasa Rais aanze kwa kuwatazama vyema hawa watendaji wake ambao amewateua katika masuaa haya ya fedha na mapato, HAWATOSHI, au achague kuendelea nao, tujikutr kwenye KINA kirefu tushindwe kujinasua..

"frasitresheni" zitaongezeka nyakati hizi, maana kati ya 12/13 December 2018 pekeee bunge la umoja wa Ulaya na bunge la senate la Marekani wameandika barua na kutoa maazimio yao katika barua hizo maazimio kuhusu hali ya kisiasa na utawala bora, demokrasia ya Tanzania tangu 2016

Bunge la senate la Marekani kupitia tume yake ya mahusiano ya nje Chini ya mwenyekiti wake Bob Corker senator wa Tennessee ameongoza tume yenye wajumbe 20 limewasilisha matakwa yake kwa Waziri wa mashauriano ya nje wa Marekani, Mike Pompeo kuhusu Hali ya utawala wa Tanzania.

Bunge la Ulaya nalo limekaa na kujadili Hali ya haki za binadamu na kupitisha azimio lake la (2018/2969) 13/12/2018 wameeleza na kutoa mapendekezo yao katika azimio hilo, wametoa masharti yao, ili waendelee kushirikiana serikali ya Magufuli. Hali ni tete sana, mambo sio mazuri.

Kumbuka; hii imekuja wakati Denmark, ambaye ni msaada mkubwa katika bajeti ya Tanzania, amesitisha msaada wake wa $10M, Benki ya Dunia wakasitisha kwa muda mkopo wake wa $300M hadi masharti yao yatimizwe, yakiwepo wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo!

Umoja wa ulaya wamemrudisha balozi wao, Brussels kwa kinachotajwa kwamba ni kujadiliana kuhusu sera na misaada ya kiuchumi yenye kuihusu Tanzania. Balozi amerejeshwa ghafla "forced departure" sasa Marekani nao wanaleta "conditions" zao, lazima 'kichwa kigonge hapa'

Bunge la Ulaya na Bunge la senate la Marekani wote wametoa maazimio yao yenye kufanana sehemu kadhaa, kama, kuwaachia wafungwa wa kisiasa, kufuta kesi za 'cyber crime' na Marekani kuleta balozi wa haki za binadamu Tanzania

Nimeona wamesema kuhusu wanasiasa kupigwa risasi kwa. Sababu ya kuikosoa serikali, kukamatwa na kufungwa magereza, vyombo vya habari kufungiwa.. Hii lazima imfanye mzee baba aoneshe HOFU, kabisa!

Bunge la senate limemtaka Waziri wa mashauriano ya nje Mike Pompeo atekeleze kwa haraka maazimio yao ikiwa serikali ya Tanzania haitaweza kufuata walichoagiza, ikiwepo kuondoa misaada yote ya Marekani Tanzania..

Noma sana.. Jaribu kufikiria tu, hawa jamaa wakiondoa misaada yao funded Chini ya mwamvuli wa USAID ikiwepo. Dawa za malaria na vyandarua na hata ARV, tutanyooka! Tunajichokonoa wenyewe..

Hivyo, Rais wangu mpendwa sana, mtukufu wetu anayo kila sababu ya msingi ya kuonekana amechoka, na akiwaomba sasa wapiga kura wake mkae chonjo kwenye vita hii ya kiuchumi.. Wengine ndio kwanza tunavuta shuka, PAMEKUCHA!

Leo nchi yetu imeingia kwenye vita na mataifa makubwa sana ulimwenguni, lazima tujitazame, wapi tumekosea. Tumedhamiria kuua upinzani ndani ya nchi, sasa tunapata upinzani nje ya nchi, na mataifa "KONKI" kabisa, ni hatari, hatuwezi hata kutoa CHANJO kwa watoto wetu sie ni TEGEMEZI 100%, Tutakaopata taabu ni wananchi!

Kweli unaweza kulala na bundi na ukaamka mwenye bahati, leo tunatembea kama kuku aliyekatwa kichwa!? Hatujui kauli gani ni sahihi.. Huyu anasema hili yule hili, bahati ni kwa wale waliokuwa wakisema "usikaze shingo, mbele pagumu"

Kwa sababu Tembo hachoshwi na pembe zake, tutaendelea kuwa wananchi wa nchi hii, tukiendelea kushuhudia GENESIS 11:1–9 ikitimiza AGANO! MAMBO MBAYA! We're now start feeling the pinch..

HIVI 2020 tunafikaje?

#MMM, Martin Maranja Masese
haya mambo yalianza kuzungumzwa kama utani sasa inaonekana kama serious hivi
 
Kuna njia kama tatu ya kujikwamua kutoka katika hili balaa..
1)Serikali ikae meza moja na Wapinzani ili kuokoa taifa
2)Serikali kukubali matakwa ya nchi wafadhili
3)Bunge lijadili uwezo wa Rais wa kuliongoza Taifa
Bunge lipi hilo mkuu, hili hili la dodoma la makofi?
 
Akili kubwa wewe! Big up. Swali langu ni moja tu; je tunavukaje hapa ili tubaki salama?!
unataka uvuke uende wapi??? au unataka uukane uafrika wako mkuu? hapa ndiyo tumefikia mwisho kabisa ndugu
 
Back
Top Bottom