Hali ni mbaya kwa Mafisadi na Wapiga Dili

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Kwa msimamo wa serikali ya awamu ya tano katika vita dhidi ya ufisadi kwa muda wa mwaka mmoja hali ni mbaya sana kwa mafisadi na wapiga Dili.

Imefikia hatua baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamepanda majukwaani na kuanza vilio ambao kwa kiingereza unaitwa (crying wolf), hivi nani alitegemea atapatikana kiongozi ndani ya ccm ambaye angeongoza vita vikali dhidi ya ufisadi kama Rais Magufuli.

Sasa hivi vilio vimeongezeka kwasababu zile fedha za haramu zinazidi kuondoka kwenye mzunguko na hata hao viongozi wa upinzani fedha waliokuwa nazo za kifisadi zimeanza kwisha.

Ndugu zangu kama nilivyosoma kwenye gazeti kuna kampuni ililipwa bilioni 60 kwa ajili ya uniform za jeshi la polisi na hizo unifomu hazikupelekwa na wala ofisi za kampuni hiyo hazijulikani kweli watanzania tunataka hali hiyo iendelee?

Mpeni ushirikiano na nafasi Rais Magufuli ili tuwe na Tanzania yenye matumaini msimkatishe tamaa. Hata hivi vyama vya upinzani vilikuwa vinajihusisha na ufisadi wasipande majukwaani kuudanganya umma. Kuna baadhi ya viongozi wao wanamiliki mali nyingi ambazo walizipata kwa njia hiyo ya kifisadi.
 
This happens only in Tanzania..... kwamba watu wakilalamikia hali ngumu ya kiuchumi wanaitwa wapiga dili! Vita dhidi ya ufisadi au matumizi mabaya ya fedha za umma, inapaswa kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi maskini na si kinyume chake. Unapoona vita ya ufisaidi na matumizi mabaya ya fedha za umma inafanya hali ya maisha ya watu wa kawaida kuwa magumu zaidi ujue something is wrong with that policy.
 
Hahahaaa, huwezi kusikia sauti ya tajiri akisema maisha magumu. Wenye maisha magumu ni walalahoi. Hivyo mnaposema mafisidi na wapiga dili mnamaanisha wananchibwa hali ya chini nsiye aliyekuwa mhusika. Umemsikia wapi dewji,bahkressa,manji,mengi,sabodo n.k wakisema hali ngumu?
 
Fisadi kuthibiti mafisadi ....

Only in Tanzania.......

Hivi tukisema fisadi mkuu ni yeye tutakuwa tumekosea? Kama rambirambi hazijulikani zimepotelea wapi kuna tofauti gani na zile akiwa wizara ya ujenzi akaulizwa bungeni ziko wapi akakosa jibu
 
Sumaye amesema serikaliyake ndioiliuza nyumba kwaiyo Magufuli asilalamikiwe.Mv DSM watengenezaji wanakifanyia marekebisho hicho kivuko tena kwagharama zao.tafutajingine la kumchafua.
 
Hivi tukisema fisadi mkuu ni yeye tutakuwa tumekosea? Kama rambirambi hazijulikani zimepotelea wapi kuna tofauti gani na zile akiwa wizara ya ujenzi akaulizwa bungeni ziko wapi akakosa jibu
pale fisadi anapopambana na fisadi
 
Lazima mtofautishe mtu anayepata pesa ama utajiri kwa njia ya halali na anayepata kwa njia ya haramu. Mfano gazeti la Forbes linalotoa taarifa ya watu matajiri duniani huwa linatoa majina ya matajiri waliojipatia utajiri kwa njia ya halali kama Bill Gates, kuna matajiri wa kiarabu wanamzidi Bill Gates lakini utajiri wao ni wa kuwaibia wananchi wanaowatawala hao huwezi kuwaangiza kwenye orodha ya matajiri. Ukiwa tajiri lazima uwe na background ya biashara yako sio kama hapa Tanzania kuna matajiri wa kifisadi ambao ndio wengi sasa hivi wana haha
 
Kwa msimamo wa serikali ya awamu ya tano katika vita dhidi ya ufisadi kwa muda wa mwaka mmoja hali ni mbaya sana kwa mafisadi na wapiga Dili.

Imefikia hatua baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamepanda majukwaani na kuanza vilio ambao kwa kiingereza unaitwa (crying wolf), hivi nani alitegemea atapatikana kiongozi ndani ya ccm ambaye angeongoza vita vikali dhidi ya ufisadi kama Rais Magufuli.

Sasa hivi vilio vimeongezeka kwasababu zile fedha za haramu zinazidi kuondoka kwenye mzunguko na hata hao viongozi wa upinzani fedha waliokuwa nazo za kifisadi zimeanza kwisha.

Ndugu zangu kama nilivyosoma kwenye gazeti kuna kampuni ililipwa bilioni 60 kwa ajili ya uniform za jeshi la polisi na hizo unifomu hazikupelekwa na wala ofisi za kampuni hiyo hazijulikani kweli watanzania tunataka hali hiyo iendelee?

Mpeni ushirikiano na nafasi Rais Magufuli ili tuwe na Tanzania yenye matumaini msimkatishe tamaa. Hata hivi vyama vya upinzani vilikuwa vinajihusisha na ufisadi wasipande majukwaani kuudanganya umma. Kuna baadhi ya viongozi wao wanamiliki mali nyingi ambazo walizipata kwa njia hiyo ya kifisadi.
Hapo kwenye RED nimepapenda, kumbe kuna viongozi wa upinzani ni mafisadi?
Kama jibu ni ndiyo, mbona tulitangaziwa kuwa mahakama ya mafisadi haina kesi hata moja?
Hao mafisadi wa upinzani,wanamhimili gani unawalinda hadi wasifikishwe mahakamani?
Halafu kumbe mama ntilie,wakulima,machinga,wenye mahoteli na wafanyabiashara za maduka ya rejareja ni wapiga dili? Maana ndo wanaolia hali ngumu.
Sikulijua hilo,ila kwa sasa nimeanza kuwachukau,kumbe ni wapiga dili...
 
Kwa msimamo wa serikali ya awamu ya tano katika vita dhidi ya ufisadi kwa muda wa mwaka mmoja hali ni mbaya sana kwa mafisadi na wapiga Dili.

Imefikia hatua baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamepanda majukwaani na kuanza vilio ambao kwa kiingereza unaitwa (crying wolf), hivi nani alitegemea atapatikana kiongozi ndani ya ccm ambaye angeongoza vita vikali dhidi ya ufisadi kama Rais Magufuli.

Sasa hivi vilio vimeongezeka kwasababu zile fedha za haramu zinazidi kuondoka kwenye mzunguko na hata hao viongozi wa upinzani fedha waliokuwa nazo za kifisadi zimeanza kwisha.

Ndugu zangu kama nilivyosoma kwenye gazeti kuna kampuni ililipwa bilioni 60 kwa ajili ya uniform za jeshi la polisi na hizo unifomu hazikupelekwa na wala ofisi za kampuni hiyo hazijulikani kweli watanzania tunataka hali hiyo iendelee?

Mpeni ushirikiano na nafasi Rais Magufuli ili tuwe na Tanzania yenye matumaini msimkatishe tamaa. Hata hivi vyama vya upinzani vilikuwa vinajihusisha na ufisadi wasipande majukwaani kuudanganya umma. Kuna baadhi ya viongozi wao wanamiliki mali nyingi ambazo walizipata kwa njia hiyo ya kifisadi.

Wanaolalamika kuhusu hali ngumu ni mafisadi au wananchi wa hali ya nchini? wewe unaropoka tu unadhani wanateseka ni wapinzani tu, ziruhusu akili zako zifanye kazi zaidi ya upeo wa itikadi za vyama. watanzania wengi siyo wana siasa
Nchi imeparangana hata shangazi yako na bibi yako kijijini wanalia je walikuwa wapiga dilii?
 
Back
Top Bottom