unaenda mazoezini na unasubiri daladala(5kms only)? ungepasha tu ndugu yangu!. yanini kuwapaka majasho wenzio!.
We jamaa kama kenge unaenda mazoezini arif unataka kupanda daladala hujui umuhimu wa mazoezi, nenda kwa jogging mkuu au unafanya mazoezi ya kichuma mboga?
watu wanajazana dar kwakua maamuzi yote makubwa yanafanyika dar mfano interview na ajira zote nzuri zina anzia dar wewe ng,a ng,ania huko bush utashangaa sisi tulio dar tunaendelea kugawana cake ya taifa
Kwa logic ya mada hii kila kitu kibaya duniani ni kwa sababu ya CCM na si watu wake, sasa mbona kwingine wameweza?Sasa kwa akili yako, London ni sawa na Dar? Dar hakuna miundo mbinu and nothing works right here in Dar Es Salaam.
Kwa logic ya mada hii kila kitu kibaya duniani ni kwa sababu ya CCM na si watu wake, sasa mbona kwingine wameweza?
Fikiria?
Mbona vichaa tupo wengi tu wakati nyie werevu mnakula vumbi!unaitaji moyo wa uwazimu au kichaa kuitetea ccm
Hivi ule mpango nilousikiaga wa kuhamishia mji mpya bagamoyo na ujenzi wa airport ya kimataifa uliishia wapi? Na ule wa kigamboni je? Daaahhh namshukuru mungu alinipaga akili zamani ya kuhama huo mji, siku hizi nikija hapo sikai zaidi ya siku 5. Mji joto, mji foleni, mji usafiri shida, mji zinaa kila kona, mji shida ya maji, kwa kweli dar sifikrii kurudi kabisa! Wacha niwe wa mkoani tu!
Sasa wewe mangi unamsema jirani yangu Masssawe ambaye hataki kuhamia Mabwe Pande, na ni mfurukutwa wa CDM.Nimegundua watu tunatofautiana sana aisee. Hizo unazoziona wewe kama kero, wenzio ndio wanazipenda! Mi kuna jamaa zangu wanakuambia hata iweje hawahami dar! Wengine hata wakipata kazi mikoani wanazikataa ili waendelee kubaki dar wakati hamna cha maana wanachokifanya. Cha ajabu kila ukiwakuta ni kulalamika tuuuu.. Mi naomba muendelee kubaki hukohuko dar ili sisi tufaidi maisha huku mikoani. By the way tunawasubiri mwezi huu mje na magari yenu ya kuazima!!