Hali mbaya ya uchumi yafuta ajira 100 TBL

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
80,836
93,625
TBL.jpg


Na MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Bia ya Tanzania Breweries (TBL), imepunguza watumishi wake takribani 100 ndani ya saa 24.

Taarifa ambazo gazeti hili limezipata kutoka kwa watumishi wa TBL, zinadai kwamba watumishi waliopunguzwa ni wale wa kitengo cha masoko.

Mtoa taarifa mmoja kutoka kwenye duru za uongozi wa TBL ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, ameliambia gazeti hili kuwa uamuzi huo ulitekelezwa Jumatatu ya wiki hii.

Alisema sababu kuu ya kupunguza wafanyakazi hao ni kulinda uchumi wa kampuni baada ya mauzo ya bidhaa kuporomoka kwa kasi katika kipindi cha mwaka jana hadi mwaka huu.

Ofisa masoko mmoja wa kampuni hiyo ambaye hajakumbwa na panga la kupunguzwa kazi, alidokeza kwamba uamuzi huo unatokana na hali ya mauzo na uchumi wa kampuni kutokuwa rafiki.

Aliongeza kuwa uamuzi wa Serikali wa kuzuia biashara ya pombe kali zinazofungashwa kwenye mifuko ya plastiki(viroba) umeathiri kwa kiasi kikubwa soko la bidhaa yao aina ya Konyagi.

“ Wameachishwa kinyama sana, waliitwa siku ya Jumatatu na kuachishwa papo hapo(on spot), wakaambiwa wayaache magari yao na kusaini fomu ya kuondoka, miye kwa bahati nzuri nimepona. Na hili jambo la viroba ndio limepigilia msumali wa mwisho,” alisema ofisa huyo.

MTANZANIA Jumamosi lilimtafuta kwa njia ya simu, Msemaji wa Kampuni ya TBL, Georgia Mutagahwa kwa ajili ya uthibitisho wa taarifa hiyo, hakupokea simu kila ilipopigiwa lakini akatuma ujumbe mfupi kuwa kabanwa na majukumu hivyo akaomba aandikiwe ujumbe mfupi wa maandishi.

Alipoandikiwa ujumbe mfupi wa maandishi juu ya madai hayo hakujibu na hata alipopigiwa tena hakupokea simu.

Kuuzwa kwa TBL

Kumekuwa na hali ya sintofahamu juu ya uhalisia wa madai ya kwamba Serikali imeishauza hisa na mali zake za Kampuni ya TBL kwa Kampuni ya Sab Miller ya nchini Afrika Kusini.

Inaelezwa kwamba uamuzi huo uliifanya kampuni ya Sab Miller kuungana na kutengeneza faida kubwa kwa pamoja na Kampuni ya Anheuser-Busch (AB) InBev ya nchini Ubeligiji.

Dadisi za mambo zinadai kuwa serikali ilidanganywa na hivyo kufikia uamuzi wa kuuza kampuni ya TBL mwishoni mwa utawala wa awamu ya nne.

“ Kuna dalili ya kwamba Serikali ya Awamu ya nne ilidanganywa kuuza hisa zake mutalab za viwanda vya bia cha TBL na mali nyingine kwa ujumla wake kwa lengo la kupata fedha lakini matokeo yake ni kujikaanga yenyewe kwa sababu iliuza TBL kirahisi na kukosa fedha nyingi kama ingekuwa na subira kuhusu mpango huo,” kiliwahi kudokeza chanzo kimoja toka serikalini.

Duru za mambo katika mifumo ya kiuchumi zinadai kuwa katika kipindi cha mwisho wa awamu ya nne, kama serikali ingekuwa kikwazo kwa uuzaji wa kila kitu kwa Sab Millier ya Afrika Kusini, kungekwamisha kuungana na Kampuni ya Kibelgiji ya Anheuser-Busch (AB) na InBev.

Inasemekana Sab Miller inamiliki hisa zaidi ya asilimia 57.5 za TBL na hivyo ndio mwenye hisa nyingi zaidi ndani ya kampuni hiyo.

Wachunguzi wa biashara na uchumi wanadai kuwa serikali ilikosa uvumilivu na hivyo kuuzwa kwa hisa zake kwa bei chee.

Muunganiko (merger) hutokea pale ambapo biashara au kampuni moja inamezwa na kampuni nyingine na kupoteza utambulisho wake kwa mwenye kuimeza na hivyo shughuli za kiuchumi huwa kubwa na hunufaika kwa ukuaji huo wa shughuli kwa kuzingatia ukubwa wake (economies of scale).

Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa AB Inbev inamlipa Sab Miller kiasi cha dola bilioni 107 na kufanya muunganiko (merger) huo kuwa mkubwa kuliko yote duniani kwenye vinywaji.

Zipo taarifa ambazo hazipata kuthibitishwa na serikali kwamba uuzwaji wa kampuni hiyo ulifanywa kimyakimya kwa mauzo ya dola zinazokisiwa kuwa ni milioni 200 ambazo wakosoaji wa uchumi wanasema kuwa ni chenji tu kwani wakati huo TBL ilimethaminishwa kwa bei ya soko ya dola billioni mbili.

Chanzo: Mtanzania
 
pole kwa walioachishwa kazi na pole kwa TBL kuuzwa ndio CCM tulioichagua Hii awamu ya mheshimiwa ikiisha tutakuwa tumenyooka kwelikweli
 
Si mzaha hali ni mbaya sana TBL ,mimi nilikua mfanya kazi wakutwa wa kampuni hiyo ila niliamua kuacha kazi mwaka jana kutokana na kudolola kwa kazi kwani kwa wiki tulikua tunaingia kazini mara tatu au hata mara moja ukizingatia siku ajiriwa hivyo mshahara wangu ulitegemea masaa niwapo kazini.Baada ya kuacha kazi nikategemea nitapata mafao yangu ila cha ajabu hadi sasa nasaga meno kudadadeki sina wa kumlaumu zaidi ya nafsi yangu kwa nini nilichelewa kuja kulima ufuta kwetu Masasi.
 
Na sie Agents tunauza Balimi tu na Mwendokasi.. Bia za 2500/- unakaa nazo ghalani mpaka unatamani uzinywe mwenyewe..
hahaha ushaona mkuu, nilishusha mzigo Fulani ukiwa na safari kama mia hivi zilishika nikakaa Nazo stock mda mrefu baadae zikaisha, saivi nashusha balimi ndogo, eagle hasa l/n, castle ndogo na Kilimanjaro plus castle lite.
 
hahaha ushaona mkuu, nilishusha mzigo Fulani ukiwa na safari kama mia hivi zilishika nikakaa Nazo stock mda mrefu baadae zikaisha, saivi nashusha balimi ndogo, eagle hasa l/n, castle ndogo na Kilimanjaro plus castle lite.
Hali ni mbaya sana mkuu.. Hizi bia kubwa unaweza hata kumtukana Mungu kwa jinsi zinavyoganda. Wakati mwingine inabidi tu ufiche mabalimi na hizi ndogo angalau kwa siku moja usogeze sogeze na hizi kubwa maana bila hivyo unaweza kulia nazo ghalani..
 
Si ajabu udhamini Wha Yanga na Simba na Kilimanjaro Tanzania music awards umepotea.
 
Afadhali...
Wakatoliki wapunguze kunywa pombe!!
Maana wanaongoza kwa Kupombeka vibaya.. Pesa yenyewe hawana!!
mtu ambae huwa angaingiza udini kwenye maongezi yake huwa namwona "trash"!! vr boring!

anyways, umesahau kipind cha mifungo za ramadhani vituo vya vitimoto na bars nyingi mauzo hudorora. cjui kwann
 
Back
Top Bottom