Hali Mbaya ya Mabenki: Mabenki sasa yawataka wenye viwanda kupunguza maombi ya mikopo

Kwani benki haziwezi kwenda kukopa BoT na kuwakopesha wazalishaji wahitajio mikopo?
 
shida sio serikali kuweka pesa zake, shida ni kwamba hela zimetoka kwenye mzunguko kwa kuzitoa pesa kwenye mabenki na kuzifungia BOT bila hata BOT yenyewe kuendeleza ukopaji kwenye sector za kibenk kama nchi zingine zinavyofanya na kuziamuru benk zilipe VAT na kodi zingine. hii ina hasara kubwa sana karibu kwa kila sector hapa nchini.
 
Mkuu umeongea facts, watanzania ni watu wa kulialia tu, Bila kuangalia ukweli wa mambo, kwanza kilikuwa na utitiri wa bank ambazo Binafsi sikuona faida zake, mimi mtu wa chini nilikuwa sikopesheki maana nikitaka kukopa ntaitishwa mavitu kibao na riba ni balaa, nikiweka laki hata mwaka hakuna faida yeyote inayoongezeka.
Asante baba Jessca kwa kuirudisha nchi kwenye mstari
 
kuna point. Umeongea hata mimi nakuunga mkono Mh.

Sote tunajua tena bila unafiki kwamba Mh Rais Wetu Ndugu Magufuli, Amefanya Kazi Nzuri sana.

Ila kwenye Eneo la Uchumi ni kweli Amepwaya na hapa Lawama zote zielekezwe kwenye Dawati lake la Washauri.

Shida ilianzia hapa kwenye Ule mpango wa kuondoa Fedha zote za serikali kwenye Mabeki ya Biashara na kuzirudisha BOT.

Hapa washauri wange mshauri Ndg Rais Kwamba Hizo Pesa ni kweli Mabenki walikua wanazitumia kukopeshea watu na kutengeneza Faida Kubwa kwenye Mabenk hayo.

Sasa hapa washauri wange mshauri Rais Azi hakiki fedha zote zilizopo kwenye Mabenki hayo.

Alafu atengeneze utaratibu wa kuingia mkataba na mabenki hayo kwamba wazitumie hizo fedha na Serikali iwe inapata Gawio kwenye Faida inayopatikana kwa mabenki hayo kinyume na ilivyokua serikali ilikuwa haipati chochote.

Mwisho. Ili kujenga Nchi nzuri na yenye uzalendo. Basi ufanyike utaratibu wa kushirikisha viongozi wote wa kisiasa na kitaaluma.

Na hapa hata ikiwezekana kwenye katiba Mpya basi kuwekwe serikali ya umoja wa kitaifa.

Ili kutuleta Watanzania Pamoja na kuondoa tifauti zetu za kisiasa kidini na kitamaduni.

Tanzania ni Nchi Nzuri Sana ikiwa sote tutawajibika kuiletea Tanzania Yetu Maendeleo.
 
Kwani benki haziwezi kwenda kukopa benki Kuu?
 
Mabenki Kufilisika ni moja ya dalili ya uchumi kukua, hapa kazi tu
 
Watumishi wa umma vp,hawakopeshwi tena?maana nilitaka kukopa mpunga wa maana
 
Asante Brigedia kwa ufafanuzi huu mzuri kwa watakaotaka kuelewa ila kwa wale wasikiliza porojo waache wabaki na porojo zao.HAPA KAZI TU.
 
Kwani hizo benki haziwezi kwenda kukopa BoT?
 
The country may face economic hardship in the very near future if deliberately and sustainable solutions could not been taken immediately to rescue this worse situation. If authority ignores, it will take years to recover our growing economy and number of destitute will increase at an alarming rates.
 
No
 
Kwani ni lazima tuige kwa wezetu? Mangapi mazuri hatuigii?
 
Bichwa uchungu kavunja usukani wa kagari ketu sasa imekua mshikemshike ndege tunduni
 
Nini kimeifanya serikali isianze kutoza riba? ukikuta nyani wanakula mahindi shambani mwako utafyeka mahindi au utatafuta namna ya kudhibiti nyani?
Utayahifadhi sehemu ambayo hao nyani hawataweza kuyapata tena
 
benki zinakopesha kupitia amana za wateja,sawa,

serikali ilikuwa mteja mkuu na ilikuwa na akaunti katika mabenki ya biashara,na ilikuwa na matrilioni ya shilingi,yalitumika kukopesha watanzania na nchi kuwa na uchumi mzuri.

Mteja huyu serikali kaamua kuweka mpira kwapani (kupeleka pesa benki kuu)wakati mechi inaendelea(mchakato wa kukuza uchumi),eti kisa mpira wa baba yake.

Mechi imevunjika(maendeleo)kila mtu kabeba vifaa vyake vya michezo anasepa,wengine wamepigwa butwaa,wengine wanambembeleza arudi game iendelee
 
Wewe utumie akili kwanza aliye Fanya banki zitegemee hela ya serikali ni CCM hiyo hiyo hivyo auna hoja ya msingi pia elewa kama umevisha nguo za kike ukaachwa kwenye watu wengi utakiwi kuzivua mana utabaki uchi ila utazivaa hadi upate za kubadilisha ndo uzivue jamaa kalivua nguo taifa kabla ya kuandaa za kubadilisha tumebaki uchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…