Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,237
- 9,867
Natumia "uchumi natural" kuelezea anguko hili la mabenki! Jamani hivi vikundi vinavyoojiita vya mchezo mf: akina mama, madereva boda boda wana fedha nyingi sana na hazipo benki, mifano ninayo...ninamiliki bodaboda na kijana wangu juzi hapa wamegawana milioni mbili kila mtu na fedha hizi alikuwa anatunza mtu tu mfukoni! Mke wangu hapa nyumbani kaweka milioni 10, eti wenzake hawataki kukopa maana sikukuu zinakaribia na wanakaribia kugawana( huwa wanakopeshana kwa riba kidogo tu)
Nini maana yake: hao nimetaja tone la maji kwenye bahari! Kuna pesa nyingi nje ya mifumo rasmi ya kibenki kwasababu benki zetu zililemazwa na hela za serikali nakuacha wajasiriamali wadogo! Ni wakati sasa wa benki kuandaa chai na soda za wateja ili kuvutia hawa watu wa chini.