Hali Mbaya ya Mabenki: Mabenki sasa yawataka wenye viwanda kupunguza maombi ya mikopo

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,130
1,500
Hayo mabenki yafungwe tu. Kwanza hayana faida kwa wananchi wengi wa kipato cha chini. Hayo mabenki yalikuwa yanafanya biashara na serikali. Yaondoke tu hayo mabenki, yafunge virago. Ikiwezekana turudi kwenye "barter system" .Tumechoka kuona wajanja wachache wananufaika na raslimali za nchi kupitia uchochoro wa mabenki wakati wananchi wengi wanateseka. Waondoke tu. Tumewachoka.
 

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,244
1,500
Sasa ni dhahiri nchi nzima tunaisoma number, hata aliyetuimbisha naye yumo
Nimeipenda hii, na hawa wafanya biashara wakubwa ni makada wakubwa wa CCM na walishangilia sana wakati babu Magu akipigishwa bao la mkono na shemejiye edo,,,
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,213
2,000
Kilio cha Waungwana waliojumlishwa kwenye dhambi za wengine naona kinasikika sasa... Kuiba waibe ccm Dhambi wanasingiziwa Wafanyabiashara,Kodi wakwepe ccm Dhambi abebeshwe Mfanyabiashara Mabaya mengi yalifanywa na ccm tunaambiwa wafanyabiashara na raia wengine ati tulizoea dili... sasa Namba inasomeka kote kote... Wale tu Pilau pale Black house wengine tunasubiri wote wachoke mambo yajipe maana sidhani kama kuna muokozi yupo atakayeweza kutuokoa
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
37,629
2,000
Hii kweli ni changamoto sana, kwa anayemshauri Rais wetu kuhusu uchumi angepigwa chini hakika...Sababu najua Mkuu wetu hajabobea ktk masuala ya uchumi bali ni anashuriwa na wachumi wa Tanzania waliopewa jukumu hili...
Nchi inapoenda siko, kila mahali vilio vilio....ni bomu linapikwa na litalipuka vibaya...na watakaoathirika ni vijana na watoto walio ktk hatua ya kukua sasa...
Tatizo mtu mwenyewe tunaambiwa hashauriki.
 
Top Bottom