KERO Hali mbaya ya barabara ya Segerea-Tabata

KERO Hali mbaya ya barabara ya Segerea-Tabata

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
590
Reaction score
706
Barabara ya Segerea-Tabata, ambayo ni miongoni mwa njia muhimu za mawasiliano katika Jiji la Dar es Salaam, imegeuka kuwa chanzo kikubwa cha usumbufu na kero kwa maelfu ya watumiaji wake wa kila siku. Ni jambo la kushangaza na la kusikitisha kuona ukarabati unaofanyika kuwa wa muda mfupi, wa kiwango cha chini na usiozingatia hali halisi ya matumizi ya barabara hiyo. Kutumika kwa viraka visivyo na kiwango katika maeneo mbalimbali, ambavyo huvunjika ndani ya miezi michache, ni ushahidi tosha wa ukosefu wa uwajibikaji, usimamizi hafifu, na uwekezaji duni wa fedha za umma.

Kama miongoni mwa wananchi ambao wana maswali ya msingi: Je, viongozi wetu wa serikali za mitaa, kata, madiwani, na taasisi kama TANROADS wapo na wanatambua majukumu yao? Je, hawafuatilii hali hii inayodhihirika kila siku kwa macho ya kila mmoja? Kukosekana kwa suluhisho la kudumu ni dalili ya ama ukosefu wa bajeti madhubuti, au matumizi mabaya ya rasilimali zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu.

Matumizi ya viraka visivyodumu yanaongeza msongamano wa magari, yanachangia ajali, yanapunguza tija ya shughuli za kila siku, na hatimaye yanafifisha jitihada za kuijenga nchi kupitia sekta ya uchumi. Hali hii ni tishio kwa usalama wa wananchi na kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kwa msingi huo, inahitajika jitihada kwa mamlaka husika kuchukua hatua madhubuti na za haraka kuhakikisha kuwa barabara ya Segerea-Tabata inajengwa au kukarabatiwa kwa kiwango cha juu, chenye kudumu na chenye kutatua tatizo la muda mrefu. Ni wakati sasa wa kuacha siasa za viraka na kuanza kufikiria maendeleo ya kweli yanayowagusa wananchi moja kwa moja.

Barabara ni uti wa mgongo wa maendeleo. Kuihudumia kwa uzembe ni kuiweka nchi njia panda. Uwajibikaji na weledi vinapaswa kuwa dira ya viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini kabisa pamoja na taasisi husika, si vinginevyo.​
 
Barabara zote za Dar es Salaam ni mbovu, zilizojaa viraka na zina mashimo.
 
Barabara zote za Dar es Salaam ni mbovu, zilizojaa viraka na zina mashimo.
Hawa serikali ya vijiji na mitaa kazi yao ni nini? Why wasifanye ufuatiliaji wa maeneo yao? Na madiwani wanakazi zipi? Yaani, sijui wanakaa kama njugu mawe tu... 😂😂😂
 
Back
Top Bottom