lacuna
JF-Expert Member
- Aug 19, 2015
- 653
- 168
HALI MBAYA UKAWA:
Hali imezidi kuwa mbaya katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kwa upande wa Ukawa baada ya chama cha mapinduzi kuweka mikakati mizuri ya ushindi,Mikakati hiyo ya CCM inewafanya UKAWA kushindwa kuwa na ushirikiano mzuri kiasi cha kila mmoja kujiangalia yeye binafsi katika eneo lake.
Kamati iliyoundwa kwa lengo la kumnadI mgombea wa urais, wajumbe wake wote wamerudi katika majimbo yao katika kuhakikisha wanashinda huku wakisema suala la urais wanamuachia mwenyewe Lowasa aangaike nalo kwani na wao wanaangalia ugali wa familia zao(yaan kila mtu afe na lake).
Kwa sasa lowasa amebaki na Sumaye pekee na hata Masha ameamua kumkimbia baada ya kusoma alama za nyakati.Aidha kwa upande wa mgombea mwenza Bw.Duni nae amechoka kuwafanyia kampeni chadema kwani takriban asilimia 95 ya majimbo anayopita kuna wagombea wa chadema kwa nafasi ya ubunge badala ya CUF,hali hiyo imemkatisha tamaa kiasi cha kufanya kampeni zake kama bora liende ili mradi tu atimize wajibu.
Aidha wagombea wa nafasi za ubunge hasa wa CHADEMA wanakabiliwa na ushindani mkubwa toka kwa CCM kutokana na namna chama hicho kilivyojipanga na pia kutumia utaratibu mzuri wa kumpata candidate wao katika eneo husika.Tofaut na vyama vya ukawa ambavyo wagombea wao wengi hawakukubaliana na utaratibu ule wa kuachiana majimbo,wengi wao ambao hawakupata wamekuwa na kinyongo kiasi cha kuhama au kufikiria kufanya hujuma ili wakose wote.
Kutokana na hali hiyo uchaguzi wa mwaka huu unaonekana utaleta matokeo ya ajabu na upo uwezekano mkubwa wale mapinzani maarufu wasirudi bungeni!Baadhi ya wabunge wanaotajwa kuja liona bunge kwa paa awamu ijayo ni Lema,Msigwa,Mkosamali,Lisu,Mnyika,Mbowe,Mbatia.Mwenyekiti wa CDM Bw Mbowe baada ya kuona hali hiyo ameamua kuondoka kwenda nje ya nchi japo kujituliza kiakili huku akijutia uamuzi alichukua wa kumkaribisha Lowasa ndani ya chama