Hali mbaya Mlima Kilimanjaro

Hapo sio Kilimanjaro wacha kutudanganya we giLESi
 
Lawama kwa serikali na wananchi hatuna utamaduni wa kutunza mazingila yetu:confused2:

Tatizo la kuyeyuka barafu mlima kilimanjaro sio la watanzania kutokutunza mazingira ni tatizo la dunia nzima. na linasababishwa na mataifa makubwa ambayo yana viwanda vikubwa. Jaribu kutafuta Global warming effects na utapata jibu.
 
Aisee mimi mbona kila siku naona barafu imefunika mlima fresh tu? Au nina PARALLAX nini?
 
Kilele cha mlima Kilimanjaro cha Kibo kipo mbali sana na Msitu ukipita upande wa Marangu Root. Miti unaicha huku Horombo Hut unakutana tu na Jangwa kubwa hadi unapofika Kibo Hut Kuelekea Kileleni. Huyu mpiga Picha hiyo miti ameipata Upande Gani wa Mlima? Hata hivyo wakati huu wa Kiangazi theluji hupungua lakini wakati wa Baridi anzia May hadi September theluji ipo ya kutosha.
Ila sehemu zile wanazoishi watu miti imekatwa kwa wingi, kahawa imekatwa na kutelekezwa. Nilisafiri kwenda Machame Hospital sikuamini Mazingira niliyokuwa nayaona. Ile Green na Maua mazuri kama ya Ulaya hakuna tena. Vijiji vimekuwa kama vya Kasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…