Hali itakuwa mbaya sana Tanzania endapo Mmarekani ataendelea kuchochea vita ulimwenguni

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,150
11,196
Kipindi ambacho vita vinanukia kule ukraine nilishawahi kuwaonya watu wasishabikie ile vita likitokea la kutokea bas hasara itakuwa ni kwetu wote na sasa mafuta yametoka 2,200 kwa sasa ni 3,500 kwa lita hii yote ni kuwa tunailipia ile vita ila kama ile vita isingekuwepo huenda lita ya mafuta ingekuwa 2400 au 2500, kungekuwa na unafuu wa maisha, ila kwa sasa hali inazidi kuwa ngumu.

Sasa Mmarekani akaona katibua kule Russia now akanja mission ya makusudi kumtarget china aingie mtegonkmi ili china aingie vitani apate sababu ya kumuharibia uchumi wake maana kwa miaka ya hivi karibuni Mchina amekuwa ni tishio kiuchumi kwa bara la ulaya na marekani nzima sasa ilikuwa inatafutwa sababu mchina aingie vitani ili marekani apate sababu ya kumbana mchina kiuchumi lakini naona mchina kashtuka.

Endapo bidhaa na makampuni ya kichina yakipigwa vikwazo vikali na china ikiingiaa kwenye vita kubwa basi tutegemee bidhaa kubwa za kichina zinazoingia hapa zitapotea kabisa maana china atakuwa vitani na meli zake zote zitapigwa pini kusafirisha mzigo popote.

Baada ya yapo tutegemee wafanya biashara wengi Tanzania kuingia kwenye umaskini mkubwa maana asilimia kubwa ya bidhaa za Tanzania kuanzia electronics hadi mavazi vinatoka china, hata hapo kariakoo ambapo ni sehem kubwa ya mapato ya TRA bidhaa aslimia 90 pale ni mchina tu, maana yake endapo mchina ataingia kwenye vita nzito basi tegemeeni wafanya biashara wataingia kwenye umaskini or kufunga kabisa maduka yao kwa kukosa bidhaa na nchi itaenda kukosa mapato makubwa.

Hizi vita kwa mtu mwenye akili hatakiwi kushabikia kabisa , hawa watu watazidi kutulietea shida.

Na njia pekee ya kupambana na haya mambao Tanzania tulishatakiwa mda mambo mengi tujitegemee wenyewe kuazia kilimo hadi kutengeneza bidhaa muhim kama vifaa vya umeme hadi mavazi, mpaka nishati.
 
Mimi huwa nawashangaa sana watu wanao furahia uwepo wa Marekani na Israel. Haya Mataifa mawili ndiyo chanzo kikuu cha vurugu, na uovu wote duniani.

Wako busy kuchochea machafuko duniani, ili wauze silaha. Hawajahi kufurahia utulivu duniani. Wamejawa na double standard! Halafu wanajiona wao pekee ndiyo wenye akili kuliko viumbe wengine.
 
THREATS TO THE WORLD PEACE
Mimi huwa nawashangaa sana watu wanao furahia uwepo wa Marekani na Israel. Haya Mataifa mawili ndiyo chanzo kikuu cha vurugu, na uovu wote duniani.

Wako busy kuchochea machafuko duniani, ili wauze silaha. Hawajahi kufurahia utulivu duniani. Wamejawa na double standard! Halafu wanajiona wao pekee ndiyo wenye akili kuliko viumbe wengine.
 
Back
Top Bottom