Hakuna utu bila uhuru wa haki bila uhuru

Hakuna utu bila uhuru wa haki bila uhuru

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Posts
899
Reaction score
1,108
Ndugu zangu Watanzania wenzangu kwa kipindi hiki ambacho chama chetu CHADEMA tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kitaifa na mimi nikiwa ni mmoja wa wagombea kwenye Nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu napenda kuongea na nyie leo maneno machache sana ila yenye uzito wake.

Kipindi changu chote cha mapambano yangu kwaajili ya uhuru wa nchi yangu, sijawahi kuwa na shaka hata mara moja kuhusu ushindi wa mwisho wa mapigano matakatifu ambayo mimi na nyie tumejitolea maisha yetu.

Kwaajili ya kile tunachoitakia nchi yetu ya kuwa na maisha ya kuheshimika yaliyo na utu yenye uhuru bila vikwazo kutoka kwenye ukoloni wa ccm na washirika wake wa kukandamiza haki na usawa kwa watakamabadiliko, Ambao wamepata msaada wa moja kwa moja ama usiyo wa moja kwa moja,kwa makusudi ama bila makusudi Maafisa Fulani wa juu wa jeshi la polisi wasiyokuwa waaminifu wameendelea kuwa upande wa ccm bila kutambua kuwa ipo siku ccm itaondoka madarakani na wao wataendelea kuwa na wajibu wakulitumika Taifa.

Wananchi wengi wanapewa rushwa kwaajili ya kufanikisha kupotosha ukweli wa uhitaji wa serikali ya ccm kuondoka madarakani,ndio Wanatuchelewesha, wanatuhuzunisha lakini ninauhakika hakuna jambo baya linaloweza kuishi milele bali jambo OVU huishi kwa muda na kupotea milele, Nenda Kenya,Malawi, Zambia nk, Kama jeshi liliwahi kushindana na Umma likashinda.

Ila Chadema hatupo peke yetu Walimu,Wakulima,Wavuvi,Madaktari,Wafanyakazi, waendesha boda boda,wasukuma mikokoteni,mama lishe,wanafunzi na wataka mabadiliko kote duniani na watu waliyohuru kutoka kila pembe ya Tanzania siku zote watakuwepo upande wa Chadema hawata utelekeza mwanga huu wa Chadema mpaka siku zitakapo kuja ambazo hakutakuwa na wakoloni tena pamoja na wanajeshi wa kununuliwa katika nchi yetu.

Kwa wenetu ambao tutawaacha na wengine ambao hatutawaona tena, Natamani waje kuambiwa kuwa mustakabali wa Tanzania ni mzuri na unatarajiwa kuwa kila Mtanzania atafanikisha kazi takatifu ya kuujenga upya uhuru wetu na utaifa wetu.

Kwakuwa bila utu hakuna uhuru,Bila haki hakuna utu na bila uhuru hakuna watu waliyo huru.

Hakuna ukatili kutendewa sivyo ama mateso yaliyonifanya niombe -kuhurumiwa kwakuwa napendelea kufa kishujaa, Imani ikiwajuu na kujiamini kwangu kukiwa na umuhimu katika kujua mwisho wa nchi yangu.

Historia itazungumza siku moja japokuwa haitakuwa historia ya kuifurahisha CCM na washirika wake kwani huwo utakuwa ndiyo mwisho wake.

Lakini ni ile itakayofundishwa kutoka mikononi mwa ccm na wapambe wake,Chadema itaandika historia yake Mwisho na itakakuwepo Kaskazini,kusini,mashariki na magharibi mwa Tanzania Historia ya utukufu na utu.

Tafadhali msisononeke makamanda wenzangu, najua mnajua nchi yetu inateseka kwakiasi kikubwa na itajua namna ya kuulinda uhuru wake....

Mgombea ujumbe kamati kuu Chadema 2014

-

Mungu ibariki Chadema

Mungu ibariki Tanzania

Mungu ibariki Afrika

Henry Kilewo

05.09.2014
 
Ni maneno ya busara na ukweli mtupu, huu uchaguzi unaendelea chadema, uzalishe chadema imara zaidi kwa ukombozi wa nchi yetu..
 
sr bachelor: hilo ndilo tumaini la kila mpenda haki mtaka mabadiliko...
 
Last edited by a moderator:
Ila Chadema hatupo peke yetu Walimu,Wakulima,Wavuvi,Madaktari,Wafanyakazi, waendesha boda boda,wasukuma mikokoteni,mama lishe,wanafunzi na wataka mabadiliko kote duniani na watu waliyohuru kutoka kila pembe ya Tanzania siku zote watakuwepo upande wa Chadema hawata utelekeza mwanga huu wa Chadema mpaka siku zitakapo kuja ambazo hakutakuwa na wakoloni tena pamoja na wanajeshi wa kununuliwa katika nchi yetu.

Hao Walimu,Wakulima,Wafugaji,Wavuvi,Madaktari,Wafanyakazi, waliopamoja na Chadema wako wapi mbona kundi la 201 BMK wamewatosa wanaendela kutunga katiba iliyo bora?

 
Naamini kwa kile ulichokinena kama kitasimama basi taifa litauona uhuru wake na wananchi watapata haki yao.
 
Wengi hupenda kukubeza kamanda Kileo ila nikuhakikishie wenye akili timamu tupo Pamojq na wewe, Maneno yako yamenigusa na kunisisimua sana.
 
Wengi hupenda kukubeza kamanda Kileo ila nikuhakikishie wenye akili timamu tupo Pamojq na wewe, Maneno yako yamenigusa na kunisisimua sana.

Hawana uwezo wa kujibu andiko la kamanda kila aandikapo zaidi ya kutukana na kupumulia mashine.
 
Hao Walimu,Wakulima,Wafugaji,Wavuvi,Madaktari,Wafanyakazi, waliopamoja na Chadema wako wapi mbona kundi la 201 BMK wamewatosa wanaendela kutunga katiba iliyo bora?

[/COLOR]

hahha,
huku ni sawa na kujitekenya na kucheka mwenyewe, unajua kuwa kundi la miambili na moja Kingunge yumo? makonda yumo?
je wameteuliw ana nani haw amakada wa chama?
 
Kuacha kumwagia watu tindikali nao ni utu.
 
kilewo katika mambo mujarabu uliyoyazunguzia katika bandiko lako La " hakuna utu bila Uhuru na Wa haki bila Uhuru" umetoa matamko dhidi ya jeshi la polisi na ccm kama kuwa wamekuwa wakiminya Uhuru Wa demokrasia isitawale kwa wapenda mabadilko ambao kimsingi wengi wao umewaona zaidi ni wale wanaipigia chapuo Upinzani,

mosi kilewo umetoa mifano kuntu yenye kuonyesha hasira yenye kuwalaumu watanzania kuwa wanahongwa na ccm kupindisha ukweli ambapo kwa upande Wangu naiona ni lugha ya ukakasi dhidi ya watanzania ambao wanajivunia UHURU ambao ni TUNU ya CCM miaka yote. kumbuka damu za mababu zetu waliopigania Uhuru huu tuojivunia sasa na Leo unakuja na hadithi zako za ABUNUASI kuwaadaa watanzania kuwa ccm yangu ni mkoloni mweusi na kuwatia hamasa yenye nia ovu kuleta mapambano dhidi ya ccm.

nataka kukushauri bwana kilewo kuwa maandishi yangu yapo ukutani kwa wino mzito na endapo damu ambazo hazina hatia zikimwagika dhidi ya mane no yako kuna mengi utakuja kuyajibu mbeleni.ni haya kwa ambayo nchi kama mifano yako wanajutia mpaka Leo nenda Kenya tazama wanavyojutia maamuzi yao mpaka kesho kwa vita vya wenyewe na damu ambazo hazina hata lepe ya hatia zikaanza kupiga kelele ardhini kuwalaumu wanasiasa walio wachochea kwa maneno ya ---- kama yako kilewo. kesho ya watanzania inawategemea wanasiasa wenye maneno ya munyu kuwatia hamasa ya kuipjgania nchi yao kujikwamua kiuchumi zaidi. kumbuka msemo usemao I YOU CAN NOT FIGHT THEM JOIN THEM.

ni hayo Machache kwa Leo


asante
 
Hawa vijana wa chadema swala la kumwagika kwa damu hawaliogopi ndio maana hawaachi uchochezi.
 
Ubaya wa wanasiasa huwa wanazungumza sana, wakati wa makunji wanawatanguliza wafuasi wao na wenyewe hawatokei. Matukio kama ya CUF Zanzibar, CDM nk yanathibitisha haya. Sidhani kama wale waliokufa Zenji huwa wanakumbukwa kwa lolote na serikali ya kitaifa na CUF .
 
Hujitambui wewe!! Kaa kimya!! Na kwanini usimjibu kwenye thread yake? Au hutalipwa kwa hiyo post hivyo unaona uanzishe mada ya kwako!? Fungua hilo tikiti uone nje ya box!!
 
Henry Kilewo na bavicha/cdm! Kwanini mnakuja hapa JF kutangaza kuwa mnagombea hapa sio sehemu ya kuomba
kura. Au ni sifa sana ukiwa mgombea ndani ya cdm??? Unatafuta huruma ya wapiga kura??

In this country Henry Kilewo you don't deserve to be a leader.....never!! Wewe na Ben mna nia OVU sana.
 
Back
Top Bottom