Hakuna ukweli kwenye maslahi ya mtu

Joined
Dec 23, 2017
Posts
35
Reaction score
69
Kama kitu hata mungu hatokusamehe ni kutumia ukweli kukandamiza maslahi ya mtu...Hii ni sawa ukamwambia mtu ile hela nimekuibia mimi ila kwa kuwa nilikuwa na matatizo...

Huwezi kuleta matatizo yako kwenye haki yangu japo ukweli nikuwa utakuwa na shida zako...Alichokifanya raisi to honest ametumia ubabe ndani ya haki ya mtumishi.....

Nani asiyejua huu ni mwaka wa tano sasa unaenda hakuna mshahara mpya nani asiyejua kuna watumishi tangu waanze kazi hawajawahi kupanda madaraja hawa nao unawaweweka upande gani...Hivi kwani sheria ya ajira inasemaje kuhusu madaraja kama hiyo haitoshi basi tuheshimu hata mikataba tu iliyopo baina ya mfanyakazi na muajiri......

Hivi hakufahamu kupanda madaraja ni haki ya mtumishi na siyo ombi muda unapofika..Hivi hakufahamu kunasheria na mikataba mbalili inayobana...Ukiangalia vyote hivyo utakuja kugundua kuna ubabe wa maamuzi.....

NINI MADHARA YAKE
1:-Motisha kushuka makazini
Katika madhara ambayo yataonekana bila kujificha ni hili la kushuka kwa ubora na utendaji kazi makazini....Huwezi ukasema mpaka umalize hiki na kile ndiyo uanze kulipa mishahara mipya.Swali dogo mtu atakalo jiuliza kwani miradi inaisha lini unakuta siyo leo wala kesho anaamua kukata zake tamaa......

2:-shughuli binafsi kuzidi
Kuanzia sasa utaona watumishi wote wataongeza nguvu na jitihada zote katika kazi zao binafsi za kujiongezea kipato..Hii inamaana hakuna tena kitu kitakacho itwa kujitolea baada ya muda wa kazi kuisha hakuna mtu atakaye kubali kubaki likizo bila kulipwa afanyeshughuli za serikali......

3:-matokeo hasi
Katika kila idara zote tusitegemee mazuri kupatikana kwani teyar utendaji kazi makazini utakuwa umeshuka sana hivyo chochote tutakachokuwa tunajaribu kukifanya hakitaleta matokeo mazuri.....

MWISHO
Nafahamu wapo wa kuu wa idara na wao watataka kutumia ubabe n.k ili kulazimisha watu wafanye kazi kwa nguvu ile ile...Niwaambie tu NDAMA AKIGOMA KUNYONYA MUACHE USIMLAZIMISHE hizi haki ni kila mmoja zinamuhusu.Huu ubabe usiokuwa na msingi ufike mwisho haki ya mtu haijengewi reli wa barabara...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…