Hakuna ubaya wowote kwa bunge kuwa dhaifu: SWOT Analysis inasema

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,373
6,756
SWOT analysis ni tathmini ambayo serikali, mashirika, makampuni, mtu binafsi hujifanyia au hufanyiwa kabla ya kuchukua hatua fulani.
Mfano Marekani na Washirika wake walijifanyia tathmini ya Swot kabla ya kupeleka majeshi Syria, wakagundua kuwa kwa mapungufu yaliyokuwepo wakati ule, wasingeweza kushinda vita.
Prof Assad baada ya kulifanyia tathmini ya SWOT bunge la JMT alibaini maeneo ambayo bunge lilikuwa na mapungufu ila nadhani kutokana na uwasilishaji akasema kuwa bunge ni dhaifu badala ya kusema kuwa bunge lilikuwa na mapungufu ambayo lingehitaji kuyafanyia maboresho.
Kwa heshima na taadhima napenda nimuombe mwalimu wangu Prof Assad ajitokeze kuboresha kauli yake kwa kuondoa neno Dhaifu na kuweka neno Mapungufu, ili bunge liweze kuchukua hatua za maboresho (continous improvement) kama inavyoshauriwa na kanuni za management science.
SWOT: Strength, Weakness, Opportunities, Threats.
images (4).jpeg
 
Nimekuelewa vyema. Hakuongea kwa maana ya udhaifu ambao spika ameutafsiri. Ameongea kitaalam kwa kutumia uzoefu wake na wa yule aliyemtangulia.

Wengi wetu tumejikita katika ushabiki wa makundi ya kisiasa, tunahangaika na personalities badala ya substance. Spika kajihisi kudhalilishwa kumbe prof pengine hakuongea kwa maana ambayo imeeleweka vibaya.
 
Back
Top Bottom