Hakuna siku ninayoiogopa kama siku ya kuoa

Hakuna siku ninayoiogopa kama siku ya kuoa

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Kwenda kuoa ,nikikaa peke yangu huwa nawaza na kufikiri juu ya siku hii kuu ambayo inabidi niipite ,tatizo mimi situmii,kilevi wala tumbaku, ni vinywaji baridi tu.

Sijui mliokwishatutangulia najua hamkufa kwani aliekufa harudi kuja kueleza machungu ya kutoka roho ndio maana tunaona kufa ni kawaida.

Shidah,nahisi huenda nikaanguka kwenye ukumbi au nitakuwa natembea mwendo wa treni ,hivi kuna ugumu gani na vipi kuuvuka ugumu huo ? Maana nimo katika kupenda ingawa kimila haturuhusiwi kumwambia wala kuzungumza nae ni wazee na pia baada yamimi kukubali kuingia kwenye dunia hiyo ya kuoana au wanandoa kama wanavyopenda kuitwa au kujiita.

Jingine linalonitisha ni hiyo siku tukishatoka kufunga ndoa ,hapo nikipakumbuka miguu inanitetemeka ,maana kama jambo hujaliona,hujalifanya ,hulijui kabisa ,wazungu wanasema first time ,face to face na ukweli ,ikinijia kuivuta hali hiyo naona naadhirika hivihivi mzee mzima.

Usiyatoshene hayo ya juu hapo kuna hili la maisha ndani ya ndoa, hili ndio napiga mahesabu mbona wengi wameoa na wanaishi na wanazaa, ila nikitaka kuruka kuingia huko mwili mzima nauona kama unayayuka na kubakia mifupa.

Maisha ndani ya ndoa hayo ila kuna hawa wanaosukuma na kukusukuma na washauri kibao wakikupa mawaiza na aya kibao, mbali ya hao kuna wale wadada hao ndio utawasikia, na wewe huoi, hivi hawa wote watakuja kukusaidia ukishaingia huko, hivi utawaona hata njia wanazopita au wakishakubandika na kupiga plaster ndio weshakutosa.

Ila kuna wale wanaokuondolea uvivu hawa wanakupa makavumkavu kama huijui dunia owah,kama maji unataka kuyaita mma ingia huko ,tuulize sisi yaani vitisho vyao ni kuponda maisha ndani ya ndoa.

Hivi wadai hapa ndani ya MMU mnayonaje hayo mambo matatu yana ukweli au ni watu kuzamishana tu ,utaambiwa maji mafupi hayo si unauwona mchanga ,unaingia kwenye maji halafu hujui kuogelea ni mgeni wa kuogelea ,unaachwa unakufa peke yako.

Niikiifikiria hii ya maisha ndani ya ndoa nakuwa kama niliepotea njia ,maana usiombe kupotea halafu huelewi lugha. Mna ushauri gani kwa hili na hayo mengine?

Kuna mmoja kapita sasa hivi ananiambia yanini kununua ng'ombe mzima wakati kilo ya nyama unaweza kununua kwenye masoko ? Ingawa sijamuelewa lakini nimemfahamu.
 
Kwenda kuwowah ,nikikaa,peke yangu huwa nawaza na kufikiri juu ya siku hii kuu ambayo inabidi niipite ,tatizo mimi situmii,kilevi wala tumbaku ,ni vinywaji baridi tu !

Sijui mliokwishatutangulia najua hamkufa kwani aliekufa harudi kuja kueleza machungu ya kutoka roho ndio maana tunaona kufa ni kawaida.

Shidah,nahisi huenda nikaanguka kwenye ukumbi au nitakuwa natembea mwendo wa treni ,hivi kuna ugumu gani na vipi kuuvuka ugumu huo ? Maana nimo katika kupenda ingawa kimila haturuhusiwi kumwambia wala kuzungumza nae ni wazee na pia baada yamimi kukubali kuingia kwenye dunia hiyo ya kuoana au wanandoa kama wanavyopenda kuitwa au kujiitah !

Jingine linalonitisha ni hiyo siku tukishatoka kufunga ndoa ,hapo nikipakumbuka miguu inanitetemeka ,maana kama jambo hujaliona,hujalifanya ,hulijui kabisa ,wazungu wanasema first time ,face to face na ukweli ,ikinijia kuivuta hali hiyo naona naadhirika hivihivi mzee mzimah !

Usiyatoshene hayo ya juu hapo kuna hili la maisha ndani ya ndoa ,hili ndio napiga mahesabu mbona wengi wameoa na wanaishi na wanazaa ,ila nikitaka kuruka kuingia huko mwili mzima nauona kama unayayuka na kubakia mifupah ! Maisha ndani ya ndoa hayo. Ila kuna hawa wanaosukuma na kukusukuma na washauri kibao wakikupa mawaiza na aya kibao ,mbali ya hao kuna wale wadada hao ndio utawasikia ,na wewe huoi ,hivi hawa wote watakuja kukusaidia ukishaingia huko ,hivi utawaona hata njia wanazopita au wakishakubandika na kupiga plaster ndio weshakutosa.

Ila kuna wale wanaokuondolea uvivu hawa wanakupa makavumkavu kama huijui dunia owah,kama maji unataka kuyaita mma ingia huko ,tuulize sisi yaani vitisho vyao ni kuponda maisha ndani ya ndoa ,

Hivi wadai hapa ndani ya MMU mnayonaje hayo mambo matatu yana ukweli au ni watu kuzamishana tu ,utaambiwa maji mafupi hayo si unauwona mchanga ,unaingia kwenye maji halafu hujui kuogelea ni mgeni wa kuogelea ,unaachwa unakufa peke yako. Niikiifikiria hii ya maisha ndani ya ndoa nakuwa kama niliepotea njia ,maana usiombe kupotea halafu huelewi lugha . Mna ushauri gani kwa hili na hayo mengine ???

Kuna mmoja kapita sasa hivi ananiambia yanini kununua ng'ombe mzima wakati kilo ya nyama unaweza kununua kwenye masoko ? Ingawa sijamuelewa lakini nimemfahamu !

Me nilifikiri unazungumzia siku ya kufa. The last day...
 
Kama hujajipanga kuoa acha kabisa subiri ukiwa tayar utaoa
 
Hujakua tayari bado ndani ya nafsi yako unajifurahisha au niseme bado una ruka ruka,ukiwa tarayi na huyo unaemtaka kumuoa ndio anaekugusa pale penyewe husikii la mzazi wala la rafiki na ndio utakua wa kwanza kutaka taree za karibu ukiambiwa bora ndoa iwe may 2015 utatoa macho na kuleta Aya nyingiiii hattaki vijiko wala upawa basi japo niowe tuu kwanza awe mke wangu... sasa basi pumzika akija yuleeee aatakae ku gusa uje useme eeeh sawa baaa?
 
Back
Top Bottom