Hakuna Rais wa Marekani aliyewahi kuyafanya haya

Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
532
Heroes don't kill innocents, they save them - Donald Trump

Kwa mara ya kwanza ndege imeruhusiwa kuruka kutoka Saudi Arabia ikaenda Israeli moja kwa moja.

Hakuna kiongozi aliyewahi kutembelea Saudi Arabia, Israeli na Vatican City katika ziara moja.

Hakuna rais aliyejitwisha mwenyewe jukumu la kwenda Israel kuongea na viongozi wa Israel na Palestina kwa dhumuni la kutafuta amani kati ya nchi hizo.

Hakuna rais wa Marekani aliyewahi kuwakusanya viongozi wa nchi za kiarabu na kuwapa vidonge vyao live kama alivyofanya Trump.

Kawakumbusha utajiri wa mali na historia walio nao waarabu. Akawaambia bara la Arabu lilitakiwa kuwa ni mahali ambapo watu wanakimbilia kupata maisha bora sio bara la watu kukimbia kiukimbizi. Na akagusia ni juu yao waarabu kuwasaidia wakimbizi wao ili wapate maisha bora.

Kawaambia asilimia 95 ya waathirika wa ugaidi ni waarabu wenyewe. Na akawaambia ni jui yao kuwakana magaidi na kuacha kuwapa misaada hasa ya kifedha. Zaidi ya hayo akasaini nao makubaliano ya kukata mifereji ya fedha ziendazo kwa magaidi.

Kawaambia ni juu yao kuchagua maisha yao ya baadae wanataka yawe ya amani na ustawi wa kiuchumi au waendelee na mateso ya ugaidi.

Hakuficha kuwa magaidi wanatumia dini vibaya. Na kila anapouliwa mtu asiye na hatia kwa jina la Mungu iwe ni tusi kwa kila muumini wa dini yeyote duniani.

Katangaza wazi kuwa lengo la Marekani ni ushirikiano, amani na uchumi bora. Akawasifu Dubai kwa jinsi walivyoiendeza nchi yao mpaka kuwa ni kituo na kivutio cha dunia cha biashara na maendeleo.

Anajisumbua kilicho moyoni mwa mtu vigumu kukitambua majibu ya ziara zake atayaona
 
Iwe kweli basi, tatizo yaweza kuwa siasa tu hapa, Saudia, Kuwait, Bahrain, Qatar na wengineo washiriki kusaidia Syri na Iraq basi, hapa ndipo napoona kama changa la macho vile...
 
Hawa Wamarekani wajanja....Wao ndio wanaowapiganisha nchi za Africa na Nchi za Arabs ili wauze silaha..
Wamarekani wanategema utajiri wao kwa kiwango kikubwa kwa kuuza Silaha..
Pia wanawapiganisha ili waibe mali kama madini n.k. Kama walivyofanya kwa Gadafi
Na sisi tusipokuwa makini tutaanza kupigana wenyewe, kwasababu ya mali tulizo nazo kama hizi wanazoiba (madini) na wanyama (twiga)
 
Ila kwanini ISIS na wanaojitoa mhanga kwa ajili ya miungu yao wanaua watu wa imani sawa na wao?
 
Hawa Wamarekani wajanja....Wao ndio wanaowapiganisha nchi za Africa na Nchi za Arabs ili wauze silaha..
Wamarekani wanategema utajiri wao kwa kiwango kikubwa kwa kuuza Silaha..
Pia wanawapiganisha ili waibe mali kama madini n.k. Kama walivyofanya kwa Gadafi
Na sisi tusipokuwa makini tutaanza kupigana wenyewe, kwasababu ya mali tulizo nazo kama hizi wanazoiba (madini) na wanyama (twiga)

Ni kweli hasa Obama na Hillary Clinton walipiganisha sana waarabu. Infact Hillary alisema hadharani kuwa lilikuwa ni wazo zuri kuwasaidia mujahidina kuondoa baadhi ya watawala ambao Marekani ilikuwa haiwataki.

Hilo ni tatizo la waarabu vilevile. Mkikubali mtu awapiganishe ni ubozi wenu wenyewe.

Trump kwa upande wake amelaani sana pesa kwa matrilioni ya dola zilizotumika kulazimisha demokrasia Arabuni. Alipinga vita ya kumuondoa Saddam.

Anasema ndani ya miaka ishirini iliyopita pesa zilizotumika kuendeshea vita Arabuni zingetosha kujenga infra structure za Marekani na kuwasaidia sana wamarekani. Badala yake zimetumika kuleta vurugu na balaa kubwa bara Arabu. Demokrasi haikupatikana na vikundi vya kigaidi vinatawala na kuhofisha usalama wa dunia.

Na ukisikiliza hiyo hotuba yake amesema huenda leo ikawa ndio mwanzo wa amani katika mashariki ya kati. Watoto walelewe na kukuwa wakiwa na amani na matumaini ya maisha bora.

Trump ana pointi sana. Ila kwa kuwa alianza kwa jeuri na kutukana wapinzani wake vyombo vya habari vya Marekani havimtendei haki hata kidogo.
 
Iwe kweli basi, tatizo yaweza kuwa siasa tu hapa, Saudia, Kuwait, Bahrain, Qatar na wengineo washiriki kusaidia Syri na Iraq basi, hapa ndipo napoona kama changa la macho vile...
Umewasahau LIBYA
 
Huyu jamaa ni mtu anaezungumza kweli, ! Hicho tu na ameonesha njia kuwa amani inawezekana pale mashariki ya kati uzuri haogopi mtu wala mfumo yupo kwa ajili ya watu! Teamtrump.......
 
Back
Top Bottom