Uchaguzi 2020 Hakuna mtu anayeweza kumpinga Lissu kwani anachozungumza hata Dkt. Magufuli mwenyewe anakikubali muda huo huo

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
457
1,973
Baada ya juzi Tundu Lissu kuibua sakata la wamachinga kuuziwa vitambulisho na kulaani kitendo hicho, Jana Rais Magufuli amelitolea ufafanuzi na kusema kuwa sio kweli na kutoa maagizo kwa wakuu wa wilaya nchi nzima kuwa ni marufuku wamachinga kuuziwa vitambulisho hivyo, Magufuli amesema kuwa hilo suala ni hiari na sio lazima.

Wakuu, hiii ndio maaana watanzania wanampenda Lissu, hakuna mtu anaeweza kumpinga Lissu kwani anachozungumza hata Magufuli mwenyewe anakikubali muda huo huo.

Hivi Kama watu wameteswa na kuumizwa Juu ya hili kwa kipindi chote cha miaka minne iweje Leo aje Lissu ndio itolewe amri? Ina maana Lissu angekuwepo Tanzania suala hili kumbe halingesumbua wamachinga, sasa wale wanaompinga Lissu wanatoa wapi nguvu ya kumpinga Lissu?
 
Kwa sasa hata miongoni mwa wanaCCM wenye akili nzuri wanajua wazi Lissu ndio mwamba wa kweli katika siasa za Tanzania, akifanikiwa kumkalisha chini Magu na wao pia wataneemeka.

Maana wao pia wamechoka kupelekeshwa kama magunia ya mahindi yaliyojazwa kwenye lori linaloendeshwa ovyo ovyo na dereva mwenye ukichaa.
 
Kwa sasa hata miongoni mwa wanaCCM wenye akili nzuri wanajua wazi Lissu ndio mwamba wa kweli katika siasa za Tanzania, akifanikiwa kumkalisha chini Magu na wao pia wataneemeka. Maana wao pia wamechoka kupelekeshwa kama magunia ya mahindi yaliyojazwa kwenye lori linaloendeshwa ovyo ovyo na dereva mwenye ukichaa.
IMG-20200922-WA0027.jpg
 
Machinga wametulia wanafanya kazi kwasababu ya JPM.akuna lugha nyingine mtu atasema na machinga wakamuelewa.
Wewe Magufuli mwenyewe ameishalijibia tiyari Kwa kusema kuwa hawalazimishwi, halafu wewe unajitekenya mwenyewe unacheka mwenywe, sasa si Magufuli angesema hivyo Au angesema manufaaa? Kwa nini aseme kuwa hawalazimishwi? Maana yake hivyo vitambulisho ni hasara na ni wizi mkubwa maana wale kipindi cha nyuma walikuwa hawalipi kodi Kwa sasahivi wanalazimika kulipa.
 
Wewe magufuli mwenyewe ameishalijibia tiyari Kwa kusema kuwa hawalazimishwi, halafu wewe unajitekenya mwenyewe unacheka mwenywe, sasa si magufuli angesema hivyo Au angesema manufaaa? kwa nini aseme kuwa hawalazimishwi? Maaana yake hivyo vitambulisho ni hasara na ni wizi Mkubwa maana wale kipindi cha Nyuma walikuwa hawalipi kodi Kwa sasahivi wanalazimika kulipa
Iwe wanalazimishwa ama hawalazimishwi point ni kwa sasa machinga wanafanya kazi kwa uhuru, tofauti na mwanzo walikuwa wanafukuzwa na mgambo na hawakutakiwa kuwepo mijini kufanya biashara.
Lissu anadandia sera za JPM hana jipya.
 
Ni nani alikuwa anawasumbua kabla ya vitambulisho! Ni Chadema?
Miaka ya nyuma machinga walikuwa wanasumbuliwa na mgambo kaja JPM kawaweka machinga kwenye uhuru na amani.sasa Lissu tawaambia nini machinga wamuelewe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom