Vodacom ndio mtandao nambari Moja kwa internet tanzania hii na hakuna mwingine tatizo lao ni gharama tu.
Kukosa internet au kuwa na internet mbovu inategemea na mambo mengi.
1. Eneo ulilopo labda ni baya au kuna watumiaji wengi wa mtandao huo kwa wakati mmoja ivyo kufanya Jam mfano unapokua dar es salaam barabara ya bagamoyo pale Morocco uwe mtumiaji wa mtandao kama wa tigo au voda kunakua na Access kidogo kwasababu ni Kama centre ya mji hivyo watumiaji ni wengi ila ifikapo usiku mtandao unakaa stable na speed ya juu kwakua watumiaji wanakua wamepungua sana.
2. Una application nyingi katika simu yako ambazo hauzifanyii updates hivyo kuwa na uzito wa kufanya kazi mfano unaingia Fb unataka angalia picha azifunguki unaweza kuta hauja updates Apk yako kwa wakati.
3. Internet setting yako haiko sawa katika simu yako kwa maana ya zile Proxy/ Network na Internet hivyo haupati internet kikamilifu
4. Simu yako ina virus wengi ikiwa una download vitu kutoka katika unsecured source uko google unapo ona kitu una downloads tu kwa kukubali inapokuja notifivmcation ya download from untrusted source.
5. Junk and Catches katika simu yako upande wa File manager kama unatumia Android kila Apk inafile linaitwa Junk and Catches izi uwa inabidi zifutwe mara kwa mara kwakua zinatengeneza mrundikano ivyo kumaliza space ya simu yako kufanya internet isifanye kazi vizuri mfano kama uko na whatsapp ukienda upande wa file Manager ukifungua utaliona ilo faile inabidi u clear.
6.Tatizo la kampuni yenyewe labda kuna itirafu ya kimtandao katika eneo ulilopo linaweza kua ni network au Mnara hivyo kama watakua watumiaji wengi wanalalamika mtandao uwa unachukua maelezo kwa wateja wanao wapigia simu na kuyawasilisha mahala husika wana na kushughulikia ipasavyo baada ya kujiridhisha mfano haujawai skia wilaya fulani simu azitoki kwenda kwa watu wa wilaya nyingine? Haya ndo matatizo ya kimtandao hivyo kampuni inapopokea simu nyingi zenye malalamiko haya hushughulikia.
KITU CHA KUFANYA
1.Piga simu huduma kwa wateja upate msaada badala ya kulalamika sana
2. Install antvirus katika simu yako kwa lengo la kupambana na virus na ku clear Files bugs.
3.updates Apk zako kila mara unapopata Notification.
4.jitahidi uwe unafuta Catches and junk katika simu yako mara kwa mara kila unapotumia.
5. Wacha kudownload kila ukionacho katika mtandao iwe nyimbo/picha au mafile ambayo haujui sources zake hapa uwa inakuja notification ya download from Unknown source wewe unakimbikia Setting kufungua unabonyeza kukubali.
6. Kila simu ina space au Capacity yake mfano kama simu memory capacity ni Gb 16 unakuta umetumia umeacha may be space ya Mb 50 au 100 hii aitakiwi inabidi uache space ya kutosha katika simu ili ifanye kazi vizuri atleast 1Gb as free space
NB. mkuu nina experience ya Call Centre na kama ukiongea na mtoa huduma asipo uliza maswali kama ayo au kupita maeneo ayo jua uyo ni mgeni ana muda mchache kwenye kazi yake au hajui kazi yake ,
Sent from my iPhone using JamiiForums