[h=1]Hakuna mgogoro CUF, zilizopo ni chokochoko M.Seif[/h]
Na Hassan Hamad
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema miongoni mwa changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi katika marekebisho ya katiba mpya ya Tanzania ni utaratibu wa kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano, ili wazanzibari nao waweze kuitumikia nafasi hiyo.
Amesema utaratibu uliopo sasa wa kumpata mgombea wa urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaikosesha fursa Zanzibar, na kutaka kuwepo ya utaratibu kwa nafasi hiyo kutumika kwa awamu baina ya bara na visiwani.
Akizungumzia kuhusu shutuma mbali mbali ndani ya Chama Cha CUF ambazo zimechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari katika siku za hivi karibuni, Maalim Seif ambaye pia ni katibu mkuu wa CUF amesema hakuna mgogoro ndani ya chama hicho bali zilizopo ni chokochoko tu.
Amesema utaratibu wa chama hicho unaruhusu kukosolewa mtu yoyote kupitia vikao vya chama na sio kupigana madongo kwenye vyombo vya habari.
kama kuna mtu mwenye hoja aziwasilishe kwenye vikao halali vya chama na sisi tutazijadili kwa kina, kwa hiyo Mheshimiwa Hamad Rashid na wenziwe kama wana hoja tutaonana kwenye vikao, na yeyote mwengine mwenye ubavu tushindane kwenye mkutano mkuu alisema Maalim Seif akionesha kukerwa na suala hilo.
Kuhusu shutuma za kumuandaa Mheshimiwa Ismail Jussa kuwa katibu mkuu wa Chama hicho siku zijazo, Maalim Seif amekana shutuma hizo na kusema kuwa wanaohusika kupendekeza nafasi hizo ni mkutano mkuu wenye wajumbe kutoka bara na visiwani.
Chama hiki si Changu, na katibu mkuu kuhojiwa ndani ya chama chetu sio tatizo, anaweza kuhojiwa wakati wowote kupitia utaratibu unaokubalika, na anayetaka nafasi ya ukatibu mkuu aje anakaribishwa wakati utakapofika, aliongeza.
......................................................................................................................................................................................................
vile vile tunahitaji Muengezeko zaidi ya wa waZanzibari kuingia katika jeshi la ulinzi la Tanzania (JWTZ) Na muengezekowa mabalozi
wa nchi za nje watokee Zanzibar.
Kama wa Tanganyika hamutakubaliana na vipengele hivyo basi Muungano huu fake utakuwa mwisho Chumbe.:A S 465: