Hakuna Mbunge Mteule, bali Rais Mteule

Asante mkuu, si wanafunzi peke yao hata watu wazima tunakumbushana!
Elimu ni bahari!
 
Pia mbunge akichaguliwa kuna kuwa hakuna mbunge mwinge aliyeko anatumiakia ubungee Maana binge linakuwa limeshavunjwa. Wakati upande wa uraisi bado raisi anakuwa madarakani kipindi raisi mteule ametangazwa

Msekwa alikosea. Kwa lugha rasmi, yeyote anayehitaji kuapishwa kabla ya kuanza kazi ni mteule. Kuchagua Spika hakubadilishi status yake ya uteule. Kwa lugha ya kawaida hakuna ubaya kumwita 'mbunge' hata kama hajaapa
 
Nyie ndo mnasababisha wanafunzi wafeli mitihani, tangu lini JF ikawa Mamlaka ya kutoa Rejea mashuleni ? Kama ni tafsiri ya maneo ya Kiswahili sitarajii kama JF ni Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Je, mwanafunzi akifanya rejea ya neno kutoka Jf kwenye majibu ya mtihani ataandika kuwa source ni JF ? Aidha, hao wana JF watakakaotoa maana ya hilo neno, una uhakika gani ni ni sawa ? Acheni kuchangia kushusha kiwango cha elimu ya Tanzania.

Nimekubali kweli akili ni nywele, kila mtu ana zake!
 
Back
Top Bottom