Uchaguzi 2020 Hakuna kulala, twendeni tukapige kura

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
340
300
Hatimaye zimebaki wiki mbili kufika tarehe 28 twende tukapige kura kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Siku hiyo ni siku ya muhimu sana kwa watanzania na inatupasa tuitumie vyema kuandika historia mpya katika nchi yetu.

Tanzania haiwezi kuendelea bila ya viongozi imara na wenye maono mapana kuhusu maendeleo ya Watanzania. Katiba ya nchi yetu inatupa fursa ya kuchagua viongozi wetu baada ya miaka mitano.

Hivyo basi ni vyema kwenda kutimiza haki yetu ya kikatiba ya kupiga kura.

Kumbuka viongozi watakaopata ushindi watapata dhamana ya kuongoza kwa miaka mitano ijayo. Viongozi hawa wakiongozwa na Rais, Wabunge na Madiwani ndio wenye jukumu la kupanga na kuamua nini kifanyike katika nchi yetu kwa miaka mitano ijayo.

Nchi yetu ipo kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lengo kuu la kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa na kupelekea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa na mawazo mbadala.

Ushindani wa kisiasa sio uadui bali ni mapambano ya hoja na sera ya nini kifanyike kwa wakati gani, kwa namna gani na kipi kitangulie kufanyika, na maamuzi haya hufanywa na wengi kupitia bunge sio na mtu mmoja .

Nchi yetu imeongozwa na chama kimoja toka tupate uhuru. Moja ya sababu ya chama hiki kuendelea kutawala ni mfumo wa nchi yetu ambao unatokana na katiba tulioyonayo kwa sasa. Katiba hii inatoa faida zaidi kwa chama tawala kuendelea kutawala.

Tukumbuke watendaji wa kuu wa tume ya uchaguzi way taifa (NEC) wote wanachaguliwa na Rais. Bahati mbaya hawa ni makada wazuri wa chama tawala na wanafanya kazi kwa kumridhisha yule aliyewateua.

Hii imepelekea sana kwa matukio mengi ya uonevu kwa vyama vya upinzani katika kipindi hiki cha kampeni. Wote tunashuhudia namna vyama hivi vinavyo nyanyaswa sana kwa madai ya kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi.

Mheshimu Tundu Lissu tayari walikwisha mfungia siku saba na sasa Halima Mdee mgombea Ubunge jim bo la Kawe kupitia CHADEMA naye anatumikia adhabu yake ya siku saba yakufungiwa kufanya Kampeni kwa toka Oktoba 12 mpka 18.

Matukio haya sio ya kushangaza kwa mtu anayefahamu mambo kwani refa yupo upande wa chama tawala na anafanya juhudi kubwa kuwatetea na kuhakikisha ushindi unaenda kwao.

Baadhi ya watanzania wamekata tamaa na hawaamini tena kwamba mambo yanaweza kubadilika katika nchi hii. Wengine hawaoni thamani ya kura zao na wanadhani kwenda kupiga kura hiyo Oktoba 28 ni kupoteza muda tuu.

Fikra kama hizo sio sawa kabisa. Twendeni tukapige kura tuonyesha kiu kubwa ya mabadiliko yaliyopo mioyoni mwetu kupitia sanduku la kura.

Changamoto wanazopata wapinzani ni changamoto zinazokabili nchi nyingi za kidemokrasia duniani.Demokrasia ya vyama vingi hasa katika nchi za Afrika zimetandwa na kuzungukwa na madhila kama haya yanayowakuba wapinzani nchini Tanzania.

Tofauti kubwa tuliyonayo na wenzetu wa nchi nyingine ni wao kusimamia na kutekeleza kwa vitendo kile wanachokiamini hasa kujitokeza kwa wingi siku ya kwenda kupiga kura.

Pamoja na mambo yote haliyotokea na yanayotokea nguvu ya mabadiliko ipo mikononi mwa umma. Nguvu yetu ipo kwenye kura na natumaini Oktoba 28 kila mmoja wetu ataenda kuonyesha nguvu yake kwenye sanduku la kura.

Changamoto kubwa ipo kwa vijana kwani vinaja wengi wanapenda kulalamika na kuilaumu serikali lakini wakati wa kufanya maamuzi wao huwa mstari wa nyuma na kulala ndani.

Vijana tubadilike siku ya kupiga kura mtaarifu na mwenzako mwende pamoja kwenda kupiga kura.

Kumbuka kupiga kura kwako kutonyesha yale yaliyo moyoni mwako na nini unachoitakia Tanzania kwa miaka mitano ijayo. Hii ni fursa kubwa kwako kuchagua kuendelea na maendeleo ya vitu ama kuchagua kwenda na maendeleo ya watu, uhuru pamoja na haki kwa watanzania wote.

Ikishapita tarehe 28 Oktoba furahsa hii haitatokea tena mpka miaka mitano ipite. Tusiogope na kuwa na mawazo kuwa tume haitatangaza matokeo ya kweli. Tutimize kwanza wajibu wetu sisi wa kwenda kupiga kura.

Ndugu yangu kumbuka kupiga kura kwako kunaonyesha yale yaliyopo moyoni mwako na kile unachokiamini ni bora na kinaifaa Tanzania kwa miaka mitano ijayo.
 
Tuombe sana!
IMG_20200218_114656_543.jpg
 
Back
Top Bottom