Hakuna kipimo cha kweli cha serikali kandamizi duniani kote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna kipimo cha kweli cha serikali kandamizi duniani kote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 13, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Katika kila tukio linalohusisha kutoelewana kati ya wananchi na serikali na kupelekea msuguano, mgogoro na ghasia tunaambiwa serikali husika ni kandamizi. Hii ni dhana potofu ni muhimu kila tukio likachukuliwa kivyake wapo pia wananchi kandamizi dhidi ya serikali. Mathalani, mwananchi anakwepa kodi au kutolipa kabisa huku akijua bila kodi serikali haiwezi kutekeleza wajibu wake. Huyu ni mwananchi kandamizi kwa maana kwamba anawakandamizi wananchi wenzake kwa kuinyima kodi serikali.

  Neno serikali kandamizi linatumiwa vibaya hata pale serikali inapofanya wajibu wake. kwa mfano, waziri magufuru ametuhumiwa kwamba yuko kwenye serikali kandamizi anapobomoa nyumba za wananchi wakati wa mipango miji lakini hata kama wananchi wamevamia hifadhi ya barabara wengi wetu tunasema hii ni serikali kandamizi. Tukiachwa bila kupanua barabara tunasema hii ni serikali isiyowajibika na kandanizi.

  Kuna wajibu wa serikali na wajibu wa mwananchi katika maendeleo ya usitawi wa jamii. mwananchi asitekeleza wajibu wake ulio ama ndani ya katiba au nje ya katiba sio mwananchi kandamizi anayewakandamiza wenzake?


  Ni sawa na ndoa sio wanaume wote ndio kandamizi wapo wanawake kandamizi. sio serikali zote ni kandamizi katika kila tukio wapo wananchi ni kandamizi kwa matendo yao dhidi ya serikali.


  Tutafakari.
   
Loading...